Na Mwandishi wetu
Mkurugenzi wa Shirika la Tanzania Media for Maritime and Fisheries Development Bwana Edwin Soko amewashauri wavuvi wadogo wa bandari ya Bagamoyo kuchangamkia fursa za mikopo ili wafanye uvuvi wenye tija.
Soko ameongea hayo kwenye ziara iliyomkutanisha na wavuvi wadogo kwenye bandari ya bagamoyo, Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani ambao wanavua kwenye Habari ya Hindi.
Baadhi ya wavuvi walitoa changamoto zao za kukosa mitaji na kujikomboa kwa kufanya uvuvi mkubwa .
Bwana Hassan Juma ambaye ni mvuvi alisema kuwa kinachomkwamisha ni kukosa mtaji wa kuwa na boti yake ya uvuvi na hivyo kuishia kuajiriwa kila Mwaka.
Pia Bwana Kombo Juma alibainisha kuwa, amekosa mtaji wa kununua nyavu ili aweke kwenye mtumbwi wake na hivyo kulazimika kuajiriwa kwa mtu mwingine.
Kufuatia kuibuliwa kwa changamoto hizo Mkurugenzi wa TMFD Bwana Edwin Soko aliwashauri wavuvi wadogo kutoogopa kukopa ili kupata mitaji ya kununua baadhi ya zana za uvuvi kwani mahitaji ya mazao ya uvuvi ni makubwa hivyo wasiopgope kukopa.
Soko aliongeza kuwa TMFD ina sera za ustawi wa wavuvi wadogo kiuchumi hivyo ina wajibu wa kumulika changamoto za wavuvi kiuchumi.
Social Plugin