Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MFANYAKAZI WA BENKI KAHAMA AUAWA KWA KUCHOMWA MOTO WA MAFUTA YA PETROLI DAR

 


Watu wasiojulikana wamemmwagia mafuta yanayodhaniwa kuwa ni Petroli na kisha kumchoma moto na kumsababishia kifo Mwanamke aitwaye Neema Towo au kwa jina jingine Martha (30) Mfanyakazi wa Bank of Africa Tawi la Kahama, Shinyanga ambaye pia alikuwa Mkazi wa kwa Mbonde, Kata ya Kwa Mathias, Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani.

Mwandishi wa habari hizi amefika kwenye Kanisa la KKKT Usharika wa Tumbi ambako leo mwili wa Martha umeagwa kisha kusafirishwa kwenda Moshi, Kilimanjaro kwa maziko ambapo Baba Mzazi wa Martha, Ndeonasia Towo amesimulia kilichomtokea Mwanae.

Mzee Towo amesema Martha alifanyiwa kitendo hicho Machi 03,2023 saa nne na nusu usiku maeneo ya Mitamba Wilayani Kibaha ambapo wahalifu hao walimpigia simu Martha akiwa Kanisani (KKKT Usharika wa Tumbi) na akatoka na kuwafuata kisha waliondoka naye na kwenda kumfanyia ukatili huo.

Mzee Towo anasema anaamini Martha hakuchomwa moto tu bali pia alichomwa dawa iliyoharibu figo zake na kuongeza kuwa Binti yake ni jasiri kwani alipambana na kukimbia akiwa ameungua hadi nyumba za jirani na kuwatajia namba za Baba yake ili wampigie ambapo baadaye Polisi walijulishwa na kumchukua hadi Hospitali ya Tumbi kwa matibabu na kuhamishiwa Muhimbili kwa matibabu zaidi na alifariki usiku wa kuamkia Alhamisi Machi 09,2023.

“Moto ule alivyokimbia usingemuua lakini kumbe waliharibu figo kwa kumchoma madawa, naomba mjifunze masuala ya simu halafu msidanganyike, Watu wa Usalama wameangalia kwenye CCTV wakamuona ametoka nje ya geti kisha ndio mwisho wake” 

Kutazama habari yote kwa urefu ingia Youtube ya millardayo.
#MillardAyoUPDATES

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com