Kikao cha Majadiliano kuondoa watoto wa Mtaani Manispaa ya Shinyanga.
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
TAASISI ya Nancy Foundation kwa kushirikiana na Serikali mkoani Shinyanga, wameanza kupanga mikakati ya kuondoa watoto wa mitaani katika Manispaa ya Shinyanga, kwa kuwakutanisha na wazazi wao pamoja na kuona namna ya kuwasaidia ili watimize ndoto zao.
Hayo yamebainishwa leo Machi 21, 2023 kwenye kikao cha kwanza cha majadiliano kuhusu watoto wa mitaani na wanaofanya kazi mitaani, kilichoshirikisha wadau mbalimbali ambao wanahusika na kutetea haki za watoto, wakiwamo Maofisa Ustawi wa Jamii, Watendaji, Viongozi Serikali za Mitaa dawati la jinsia na mashirika yasiyo ya kiserikali.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Nancy Foundation Ezra Manjerenga akizungumzia mpango huo, amesema walifanya utafiti na kuona kumekuwepo na tatizo la watoto wengi mitaani katika Manispaa ya Shinyanga wakidhurura na kuomba hovyo, ndipo wakaona ni vyema washirikiane na Serikali kuwasaidia watoto hao na kuwaondoa mitaani.
“Hakuna mtoto wa mitaani kila mtoto ana wazazi wake, na watoto ni baraka na zawadi kutoka kwa mungu, kwanini leo wanaachwa hovyo mitaani, sisi tutazungumza na watoto hawa ili kuona wanakabiliwa na tatizo gani na kisha kuona namna ya kuwasaidia na kuishi kama watoto wengine na kuendelea na masomo yao,” anasema Manjerenga.
“Program hii itakwenda muda wa miezi mitatu na baada ya hapo tutaona mafanikio ambayo yamepatikana, kisha tutaendelea nayo tena hadi kuhakikisha hakuna mtoto ambaye anadhurura hovyo mitaani,”anaongeza Manjerenga.
Naye Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Shinyanga Lidya Kwesigabo, amesema tatizo hilo la watoto wa mitaani lisipo dhibitiwa mapema linaweza kutokea tatizo kubwa likiwamo wimbi la vibaka.
Aidha, ametaja takwimu za watoto wa Mitaani kwa Mkoa mzima wa Shinyanga kuwa wapo 612, na jumla ya watoto ambao wanaishi katika mazingira hatarishi ni 99,939 na kutaja baadhi ya sababu zinazosababisha watoto kuishi mazingira hayo ni migogoro ya ndoa, umaskini, malezi duni, mazoea ya kuishi mitaani, na uvutaji wa madawa ya kulevya.
Nao wadau hao wa maendeleo wamepongeza programu hiyo ya kuondoa watoto wa mitaani, na kuahidi kutoa ushirikiano wa kutosha, ili watoto hao waishi kwa upendo na kuendelea na masomo yao.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Nancy Foundation Ezra Manjerenga akizungumza kwenye kikao hicho.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Nancy Foundation Ezra Manjerenga akizungumza kwenye kikao hicho.
Afisa Ustawi wa Jamii Lidya Kwesigabo akizungumza kwenye kikao hicho.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Yudas Ndugile akizungumza kwenye kikao hicho.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho.
Social Plugin