Na Woinde Shizza,ARUSHA
Imebainika kuwa ugonjwa wa saratani hapa nchini umeonekana kuwa tatizo linaloongezeka kila mwaka hususani saratani ya mlango wa kizazi wa wanawake kwani kati ya wagonjwa 100 wenye saratani za aina mbalimbali wagonjwa asilimia 47% wanakutwa na saratani ya mlango wa kizazi.
Hayo yamebainishwa na meneja wa huduma ya kinga ya saratani kutoka Taasisi ya Ocean road Dr.Maguha Stephano wakati akiongea na mwandishi wa habari hizi katika hospitali ya rufaa ya mkoa ya Mount Meru sehemu ambayo wameweka kambi maalum ya uchunguzi na matibabu ya saratani huduma ambazo zinatolewa na madaktari bigwa wa saratani kutoka taasisi hiyo bure .
Alisema kuwa kati ya wanawake 100 wenye magonjwa ya saratani za aina mbalimbali ikiwemo saratani ya mfumo wa chakula (koo)na saratani ya matiti , asilimia 47% ya wagonjwa wanasaratani ya mlango wa kizazi.
Alisema kuwa saratani ya mlango wa kizazi ndiyo inaongoza hapa nchini kwa kusababisha wagonjwa wengi ,pamoja na vifo ambavyo vinatokana na ugonjwa wa huo ,hivyo aliwataka akina mama wajitokeze kwa wingi kufanyiwa uchunguzi wa awali ambapo alisema kinachotia moyo ni mabadiliko ya awali ya chembembe hai zilizopo katika mlango wa kizazi yanatibika kabisa .
“Tupo hapa na wagonjwa ambao tutawabaini wana mabadiliko ya awali tunawapa matibabu ya awali ya saratani ya mlango wakizazi na tangu tuanze kutoa huduma hii kwa apa Arusha juzi (jana) tumewagundua akina mama wanne wana viashiria ya mabadiliko ya awali ya saratani ya mlango wa kizazi kwa iyo tumeshawapatia tiba kwa hiyo tuna uhakika pia tumewakinga lakini pia tuna wamama watano tumewakuta wana viashiria ya kuwa wanasaratani ya mlango wa kizazi kwa iyo tumechukuwa vinyama kwenye mlango wa kizazi tunavifanyia uchunguzi kwa sababu pia tumekuja na madaktari bigwa wa kuchunguzi wa sampuli za vinyama au majimaji /damu mwilini kuangalia uwepo wa chembechembe za saratani (Patholojia)kwa hiyo pia majibu watapata na wakithibitika kweli wana tatizo hilo tutawapeleka Ocean Road kwa ajili ya matibabu”, alisema Dr. Maguha.
Aidha alisema kuwa saratani ambayo inafuatiwa kwa kusababisha vifo vya wanawake wengi ni saratani ya matiti ,ambayo ndiyo inashika namba mbili na ya tatu ni saratani ya koo la chakula ambapo alifafanua kuwa hizi ndiyo saratani ambazo zinashika kasi na zinasababisha sana vifo vingi vya kina mama vinavyotokana na ugonjwa huo.
“Hatukuwaacha wababa nao pia tunawapa huduma na kwa upande wa kinababa saratani ambayo inaonekana ina wagongwa wengi sana kwa takwimu zetu za taasisi ya ocen road kwa mwaka uliopita ni saratani ya koo la chakula ndio inaongoza ikifuatiwa na saratani ya tezi dume ambayo hii inaadhiri wakina baba wengi lakini pia kusababisha vifo vinavyotokana na saratani kwa kina baba na niseme hizi saratani zote nilizozitaja zina kinga yake na pia zina fanyiwa uchunguzi na ndio maana tup o hapa kufanya uchunguzi wa awali na kuweza kutoa matibabu ya awali ya mabadiliko ya sawali ambapo wakina mama wataonekana wa mabadiliko ya saratani ya mlango wa kizazi", alisema Dr. Maguha.
Alisema kuwa kisababishi kinachosababisha wanawake wengi kupata saratani hii ya mlango wa kizazi ni kirusi kinachoitwa pactheloma ambacho kinasambazwa kwa njia ya kujamiana ambapo mwanamke anapokutana na mwanaume mwenye maambukizi ya kirusi hicho ndio anapopata maambukizi na baada ya muda mrefu maana tafiti zinaonyesha baada ya maambukizi ya kirusi hicho inaweza ikachukua hata miaka 10 au kumi na tano mwanamke huyo kujigundua ,hivyo aliwashauri pia wanawake kuwa na mazoea ya kwenda kupima afya zao mara kwa mara.
Alitaja baadhi ya vihatarishi vinavyompelekea mwanamke kupata hicho kirusi ni pamoja na wasichana kuanza kufanya ngono katika umri mdogo ambapo alifafanua kuwa kwa kufanya hivyo kunamuweka hatarini msichana kupata saratani hii, aidha aliongeza kuwa kuwa na mahusiano na wanaume wengi pia ni hatari pamaja na kuwa na mwanamme mwenye uhusiano na wanawake wengi pia ni hatari .
Aliwataka akina mama kujitokeza kwenda kupima saratani hii kwani haichukui muda ,pia ni rahisi ambapo alibainisha kuwa matokeo ya uchunguzi ni mazuri kwakuwa iwapo ukigundulika una tatizo utapewa tiba ya awali ikiwemo ile ya kugandisha ambayo inazuia chembe chembe hai zisiendelee kubadilika kuwa saratani lakini ukibainika pia una saratani wakati wa uchunguzi itakuwa ni vizuri maana utakuwa umeiwahi saratani ya mlango wa kizazi inatibika kabisa endapo itapatiwa matibabu mapema.
Social Plugin