Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa Sh.milioni 10 kwa ajili ya kuwawezesha Wanawake wa Vikundi mbalimbali vya vicoba wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
Akizungumza wakati akikabidhi fedha hizo Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Dodoma Mhe. Mariamu Ditopile amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatambua jitihada za wanawake nchini katika kazi wanazozifanya kuhakikisha wanajikwamua kiuchumi.
“Rais Dkt. Samia anawapenda sana wana Kondoa na wakati nakuja hapa niliwasiliana nae akanikabidhi Sh.Milioni 10 na amesema fedha hizo zikabidhiwe kwa vikundi vya vicoba zikawasaidie wanawake kujiimarisha kiuchumi",amesema.
Social Plugin