Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAJI SHINYANGA


Kamati ya Maji na Mazingira ikitembelea tanki la maji ya Ziwa Victoria toka Tinde mkoa wa Shinyanga kwenda Shelui mkoa wa Singida
Wajumbe wa kati ya maji wakiwa tanki la maji ya Ziwa Victoria toka Tinde mkoa wa Shinyanga kwenda Shelui mkoa wa Singida
Meneja wa RUWASA wa mkoa wa Shinyanga Eng.Julieth Payovela akitoa maelezo mbele ya Kamati ya Bunge ya Maji na Mazingira katika mradi wa maji ya Ziwa Victoria unaotekelezwa kijiji cha Shishinulu kata ya Isaka
 Naibu Waziri wa Maji Maryprisca Mahundi akiongea katika kijiji cha Shishinulu kata ya Isaka wakati Kamati ya Bunge ya Maji na Mazingira ikikagua miradi ya maji.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maji na Mazingira Jackson Kiswaga akiongea na wananchi wa kijiji cha Shishinulu kata ya Isaka wilaya ya Kahama walipokwenda kukagua mradi wa maji ya ziwa Victoria toka Kagongwa , Kahama wenye thamani ya shilingi bilioni 4.256 .
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maji na Mazingira Anna Lupembe akiongea na wananchi wa Shishinulu walipokwenda kukagua mradi wa maji ya ziwa Victoria toka Kagongwa kwenda Kata ya Mwalugulu na Isaka.
Kamati ya Bunge ya Maji na Mazingira wakiwa katika kijiji cha Shishinulu kukagua ujenzi wa mradi wa maji ya ziwa Victoria toka Kagongwa , Kahama hadi Shishinulu kata ya Isaka linapojengwa tanki la maji.

Na Patrick Mabula , Kahama.


Kamati ya Bunge ya Maji na Mazingira imeeleza kuridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi ya maji inayotekelezwa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) mkoa wa Shinyanga kupeleka maji katika vijiji vya kata za Mwalugulu na Isaka wilayani Kahama.


Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mbunge Jackson Kiswaga leo Jumatano Machi 15,2023 baada ya kukagua miradi ya maji ya Ziwa Victoria kutoka Kahama kwenda vijiji vitano katika kata ya Mwalugulu na Isaka wilayani Kahama yenye thamani ya shilingi bilioni 4.256.

Akiongea baada ya kukagua utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji ya ziwa Victoria kuyatoa Tinde mkoa wa Shinyanga kwenda Shelui mkoa wa Singida wenye thamani ya shilingi bilioni 24.47 unaotekelezwa na Serikali Kiswaga amesema utekelezaji wake umeshaanza.


Kiswaga amesema Kamati yake ya Bunge ya Maji na Mazingira imeridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo ya fedha zinazotolewa na Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha anawatua ndoo kichwani akina mama na jamii katika kupata maji safi na salama.

Wajumbe wa kamati hiyo wakiongea kwa nyakati mbalimbali wametoa ushauri kwa Serikali mahali ambapo miradi ya maji inajengwa kuhakikisha wananchi wanaozunguka maeneo hayo wanapatiwa huduma ya maji ili waweze kuitunza na kuilinda vizuri pamoja na vyanzo vya maji .

Awali meneja wa RUWASA wa mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Julieth Payovela amesema katika utekelezaji wa mradi wa maji toka Kagongwa kwenda kata za Isaka na Mwalugulu umeshindwa kukamilika kwa wakati kutokana na changamoto ya upatikananji wa mabomba ya chuma.

Naye mkurugenzi wa mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)  , Mhandisi Yusuph Katopola akiongea mbele ya kamati hiyo katika tanki la maji lenye ujazo wa lita 1,150,000 katika kata ya Tinde kupeleka Sherui mkoa wa Singida amesema utekelezaji wake unakwenda vizuri ambapo linanufaisha vijiji 22 na watu 60,000 kupata maji safi na salama.

Kamati hiyo ya Bunge ya maji na mazingira imeshauri katika miradi yote ya maji kuwepo na ushirikishwaji wa wananchi ili kuhakikisha wanaitunza na kuilinda miundo mbinu ya maji iweze kudumu na kuwanufaisha kwa mda mrefu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com