Mwakilishi wa Ubalozi wa Finland Juhana Lehtinen akizungumza kwenye Chuo cha VETA wilayani Kishapu walipokitembelea kuona utekelezaji wa mradi wa chaguo langu haki yangu.
Na Marco Maduhu, KISHAPU.
UBALOZI wa Finland Tanzania umetembelea Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) wilayani Kishapu, ili kuona utekelezaji wa mradi wa chaguo langu haki yangu.
Mradi huo unasomesha mabinti ambao wanakabiliwa na mazingira magumu, wakiwemo waliofanyiwa ukatili na kupewa mimba za utotoni, pamoja na mabinti wenye ulemavu, ambao unatekelezwa na WiLDAF kupitia Shirika la umoja wa mataifa la idadi ya watu UNFPA kwa ufadhili wa Ubalozi wa Finland.
Akizungumza leo Machi 23,2023 Mwakilishi wa Ubalozi wa Finland kwenye Chuo hicho cha VETA wilayani Kishapu Juhana Lehtinen, amesema amefarijika kuona namna mabinti wanavyopata mafunzo ya ufundi, ambayo yatabadilisha mfumo wa maisha yao, ziara ambayo ilienda sambamba na ufunguzi Rasmi wa Programu hiyo ya chaguo langu haki yangu.
"Tumekuja hapa VETA wilayani Kishapu kuona namna utekelezaji wa mradi wa chaguo langu haki yangu unavyotekelezwa na kusaidia mabinti ambao wamefanyiwa ukatili na wengine kupewa mimba za utotoni, nimefurahi kuona unatekelezwa vyema na mabinti wanapata ujuzi,"amesema Juhana.
Naye Mshauri wa masuala ya jinsia kutoka UNFPA Maya Hansen, amewataka Mabinti hao, fursa ambayo wameipata waitumie vizuri katika kuleta chachu ya mabadiliko katika maisha yao.
Aidha, Mkurugenzi wa WiLDAF Anna Kulaya, amesema mradi huo wa chaguo langu haki yangu ni jumuishi, ambao unahusisha pia mabinti wenye ulemavu kwa ajili ya kusomeshwa mafunzo ya ufundi stadi bure na kupata ujuzi ambao utawasidia kuendesha maisha yao bila ya utegemezi.
Kwa upande wake Mgeni Rasmi Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan katika utawala wake amelipa kipaumbele suala la elimu na kutoa fedha kwa ajili ya kujengwa vyuo vya ufundi stadi VETA ngazi ya wilaya.
Amewapongeza wadau hao wa maendeleo kwa kuwafadhili mabinti hao, na kuwasomesha bure mafunzo ya ufundi ambayo yatatimiza ndoto zao zilitotaka kukatishwa, ikiwamo kupewa ujauzito pamoja na wenye ulemavu kunyimwa fursa ya kusoma.
Mkurugenzi wa Mafunzo kutoka VETA Makao Makuu Abdallah Ngodu akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa VETA, amesema vyuo vya VETA vina fani zaidi ya 90, na Serikali imekuwa ikitoa fedha kuendelea kujenga vyuo ili vienee kila wilaya, na kubainisha kuwa Rais Samia ameshatoa tena fedha kujenga Vyuo vingine 65.
Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga Magu Mabelele ambaye pia ni msimamizi wa Chuo cha VETA wilayani Kishapu, amesema walipokea mabinti 240 kutoka Shirika la WiLDAF wakitokea wilaya ya Kahama, Kishapu na Butiama, na sasa wanaendelea na mafunzo ya ufundi katika fani mbalimbali.
Nao Mabinti hao kwa nyakati tofauti wamewashukuru wafadhili hao, kwa kuokoa ndoto zao ambazo zilikuwa tayari zimeshapotea, lakini kwa sasa wanakwenda kuzitimiza na kuahidi kujifunza kwa bidii, ili kupata ujuzi ambao utakuwa mkombozi wa maisha yao.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza kwenye uzinduzi wa mafunzo ya muda mfupi ya utekelezaji wa mradi wa chaguo langu haki yangu kwa mabinti.
Mwakilishi wa Ubalozi wa Finland Juhana Lehtinen akizungumza kwenye Chuo cha VETA wilayani Kishapu walipokitembelea kuona utekelezaji wa mradi wa chaguo langu haki yangu.
Mshauri wa masuala ya jinsia kutoka UNFPA Maya Hansen akizungumza kwenye ziara hiyo pamoja na ufunguzi wa Program ya mafunzo ya utekelezaji wa mradi wa chaguo langu haki yangu.
Mkurugenzi wa Shirika la WiLDAF Anna Kulaya akielezea namna wanavyotekeleza mradi huo wa chaguo langu haki yangu kwa mabinti katika vyuo vya ufundi stadi VETA.
Mkurugenzi wa Mafunzo kutoka VETA Makao Makuu Abdallah Ngodu, akizungumza kwenye ziara hiyo na ufunguzi wa mafunzo ya muda mfupi kwa mabinti kupitia mradi wa chaguo langu haki yangu.
Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Mgharibi Asante Rabi akizungumza kwenye ziara hiyo na ufunguzi wa mafunzo ya muda mfupi kwa mabinti kupitia mradi wa chaguo langu haki yangu.
Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga Magu Mabelele ambaye pi ni msimamizi wa Chuo cha VETA wilayani Kishapu akielezea namna wanavyotoa mafunzo kwa mabinti hao kupitia fani mbalimbali ambazo wamezichagua.
Mmoja wa Mabinti akitoa shukrani kwa wafadhili kuwasomesha mafunzo ya ufundi na kutimiza ndoto zao.
Meza Kuu wakiwa kwenye hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya muda mfupi na kuona utekelezaji wa mradi wa chaguo langu haki yangu.
Mwakilishi wa Ubalozi wa Finland Juhana Lehtinen(kushoto) akiwa na Mshauri wa masuala ya jinsia kutoka UNFPA Maya Hansen kwenye ufunguzi wa mafunzo ya muda mfupi na kuona utekelezaji wa mradi wa afya yangu chaguo langu.
Mkurugenzi wa Mafunzo kutoka VETA Makao Makuu Abdallah Ngodu (kushoto) akiwa na Afisa kutoka Shirika la WiLDAF Bi Joyce kwenye ufunguzi wa mafunzo ya muda muda mfupi na utekelezaji wa mradi wa chaguo langu haki yangu.
Wadau wakiwa kwenye chuo cha VETA wilayani Kishapu.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akikata utepe kuzindua Program ya mafunzo ya muda mfupi wa utekelezaji wa mradi wa chaguo langu haki yangu kwa mabinti hao.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akikata utepe kuzindua Program ya mafunzo ya muda mfupi wa utekelezaji wa mradi wa chaguo langu haki yangu kwa mabinti hao.
Mambinti wakisikiliza Nasaha mbalimbali kutoka kwa wageni ambao ni wafadhili wao wa mafunzo ya ufundi stadi na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Mabinti wakiendelea kusikiliza Nasaha za wageni na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Mabinti wakiendelea kusikiliza Nasaha za wageni na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Wafadhili wakiangalia namna mabinti wanavyopewa mafunzo ya ufundi stadi kupitia mradi wa chaguo langu haki yangu unaotekelezwa na UNFPA Pamoja na WiLDAF kwa ufadhili wa Finland.
Mabinti wakiwa kwenye darasa la ushonaji nguo katika Chuo Cha VETA wilayani Kishapu wakiwa wametembelewa na wafadhili wao.
Mabinti wakiendelea na zoezi la kujifunza kushona nguo.
Wafadhili wakiangalia namna Mabinti wanavyojifunza kushona nguo.
Mabinti wakiendelea na zoezi la kujifunza kushona nguo.
Mabinti wakiendelea na zoezi la kujifunza kushona nguo.
Mabinti wakiendelea na zoezi la kujifunza kushona nguo.
Mkurugenzi wa Mafunzo kutoka VETA Makao Makuu Abdallah Ngodu, (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Shirika la WiLDAF Anna Kulaya.
Ziara ikiendelea katika Chuo cha VETA wilayani Kishapu kuona namna utekelezaji wa mradi wa chaguo langu haki yangu jinsi mabinti wanavyofundishwa ufundi katika fani mbalimbali.
Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya kumalizika kuzinduliwa Rasmi Program ya mafunzo ya muda mfupi kupitia mradi wa chaguo langu haki yangu.
Mkurugenzi wa Shirika la WiLDAF Anna Kulaya akipiga picha ya pamoja na Mabinti hao.
Mkurugenzi wa Shirika la WiLDAF Anna Kulaya akipiga picha ya pamoja na Mabinti hao.
Social Plugin