Tarehe 10 February 2023 Taasisi ya Holysmile ilizindua Mpango kuelekea tamasha la Usiku wa Tuzo za wadau Shupavu msimu wa pili Wilaya ya Shinyanga kwa wadau mbalimbali Wilaya ya Shinyanga (SHY MC, SHY DC). Mkurugenzi wa Holysmile Bwana Bweichum ametoa ufafanuzi kwanini taasisi imeamua kuleta tuzo hizi katika Manispaa ya Shinyanga.
HolySmile ni taasisi inayotoa huduma za Sanaa, Utamaduni na Burudani Pamoja na kutambua na kuthamini juhudi na harakati zinazofanywa na wadau wote wa maendeleo iliyosajiliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa namba BST/00278 Taasisi ya HolySmile imeandaa tamasha la utoaji tuzo (SHINYANGA MDAU SHUPAVU AWARDS) litakalofanyika tarehe 31.03.2023, kwa kushirikiana na kitengo cha Utamaduni, Sanaa na Michezo Pamoja na vitengo vyote vya halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na Halmashauri ya Shinyanga Vijijini na wadau mbalimbali wa maendeleo.
SHINYANGA MDAU SHUPAVU AWARDS ni hafla ya kijamii iliyoandaliwa na Taasisi ya HolySmile yenye lengo la kutambua na kuthamini vipaji au juhudi zinazofanywa na watu binafsi au vikundi katika kategoria tofauti ndani ya Wilaya ya Shinyanga ambazo zinachochea maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kiutamaduni ni tamasha endelevu litakalo kuwa likifanyika kila mwaka ikiwa Huu ni Msimu wa pili ambapo tamasha lililopita lilifanyika Tarehe 08/12/2021 Manispaa ya Shinyanga.
kwa msimu huu wa pili taasisi itatoa tuzo 35 kama ilivyoainishwa hapo chini na tuzo 5 za heshima ambazo hazitoshindaniwa.
ORODHA YA VIPENGELE VYA TUZO
1. Best Female Public Influencer.
2. Best Male Public Influencer.
3. Best Male Mc
4. Best Female Mc
5. Best Photographer
6. Best Decorator.
7. Best Catering.
8. Best Cakes Services Provider
9. Best Makeup Artist.
10. Best Tailoring & Clothing Design Service Provider
11. Best Newspaper Journalist.
12. Best TV Reporter.
13. Best Media Personality
14. Best Videographer.
15. Best DJ
16. Best Gospel Music Artist
17. Best Gospel Music Group
18. Best Music Producer
19. Best Entrepreneur Group.
20. Best Clean ward
21. Best Bar.
22. Best Hotel.
23. Best Barbershop.
24. Best Bongo Flava Musician.
25. Best Hip-Hop Musician
26. Best Actor
27. Best Actress
28. BEST ENTERTAINMENT GROUP
29. Best Female Miner.
30. Best Male Miner.
31. Best Restaurant Service Provider.
32. Best Entrepreneur
33. Best Upcoming Entrepreneur
34. Best Male Business Influencer.
35. Best female Business Influencer.
Tuzo za Mdau Shupavu ni tuzo endelevu za mara moja tu kwa mwaka kwa kila Wilaya na Mkoa, ingawa aina za tuzo, uteuzi wa washiriki na upigaji kura utaanza mapema. Kama waandaaji wa hafla jukumu letu ni kuangazia na kuonyesha kategoria tofauti kwa hadhira ili waweze kuteua au kupendekeza washiriki wanaofikiria wanafanya vizuri zaidi katika kategoria zao ambapo mapendekezo yalifanyika rasmi kuanzia tarehe 10 FEBRUARY 2023.
KWA NINI TUNATOA TUZO?
- Kutambua na kuthamini juhudi za washika dau katika kuchochea na kuleta maendeleo chanya katika Jamii kupitia Huduma zao.
- Kufungua fursa za uwekezaji na ukuaji wa Biashara Kuweka upya Wadau Shupavu kwa ushindani wa kibiashara na masoko ndani na nje ya Mikoa ya Kanda ya ziwa.
- Kuhimiza/ kuhamasisha shughuli na kuongeza thamani ya maendeleo ya kijamii, kiuchumi, elimu, afya na kiutamaduni na Sekta zote .
- Kutangaza Fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya Wilaya, Mikoa na Taifa.
- Kuhamasisha Wadau katika Kujitoa katika Shughuli za Kijamii.
- Kuwaibua wadau Wapambanaji Katika Kila Wilaya na Mkoa na kuwafanya Wafike ngazi ya Taifa kwa kutambua na kusherehekea mafanikio ya Wadau katika Sekta Mbalimbali za Maendeleo.
- Kuwepo na ukuaji wa soko lenye ushindani na Bidhaa Bora.
- kutengeneza mahusiano mapya kati ya Mdau Mmoja na Mwingine.
- kuwapongeza wadau mbalimbali waliofanya vizuri katika Kuleta maendeleo katika Jamii kwa kuwatunuku tuzo maalumu za kushindaniwa, Takwimu na Heshima.
UTARATIBU WA KUMPIGIA KURA MDAU SHUPAVU 2022/2023 SHINYANGA
MFUMO WA KUPIGA KURA KWA NJIA YATOVUTI | holysmile.org/voting |
BONYEZA: holysmile.org/voting
JAZA MAJINA YAKO MAWILI
WEKA NAMBA YAKO YA SIMU
MAHALI ULIPO
CHAGUA CATEGORY
CHAGUA MSHIRIKI UNAEMPIGIA KURA
MWISHO BONYEZA NENO SUBMIT
MFUMO WA KUPIGA KURA KWA NJIA YA WhatsApp
______________________
Andika jina lako na Jina la Mshiriki na Kipengele anacho shiriki
kupitia WhatsApp kwenda+255 622 891 972
Mwisho wa kuchagua ni Tarehe 25.03.2023 Saa 6:00 Usiku
· Kura zitapigwa kwa siku 18 Kuanzia leo Tarehe 07 hadi 25 March 2023. Mwishoni mwa Mchakato wa Upigaji Kura, Wakaguzi watakusanya kura na kuwasilisha matokeo yaliyotiwa muhuri kwa mtayarishaji wa tuzo siku kuu ya sherehe. Wateule walio na idadi kubwa zaidi ya kura katika kila kitengo ndio watashinda tuzo.
· Baada ya Kura kupigwa na kupitia matokeo tarehe 31.03.2023 itafanyika hafla kubwa ya kukabidhi tuzo hizo kwa washindi.
Uongozi wa taasisi unaomba wadau wa maendeleo Wilaya ya shinyanga kujitokeza kwa wingi kufadhili zoezi hili ili kuweza kufanya kwa ufanisi na jambo hili kuwafikia watu wengi.
Ili uweze kushiriki usiku wa tuzo za Mdau Shupavu kwa gharama ya Kawaida 30,000 , VIP 50,000 ,watu wawili na Meza VVIP 300,000 kwa watu watano ambapo itajumuisha chakula na vinywaji. Kama utapenda kuwa sehemu ya Udhamini wa Usiku wa Tuzo za wadau chagua kifurushi cha ufadhili hapo chini.
FAIDA ZA UFADHILI
Huduma Yako Itapata Faida Zifuatazo Baada ya kufadhili;
1. Tutakuwa na wadau mbalimbali kutoka sekta mbalimbali kama wafanyabiashara, wakulima, wafugaji, mameneja na maofisa kutoka taasisi mbalimbali, wawekezaji, viongozi wa Serikali, Wabunge na watu mashuhuri. Hivyo Huduma yako itapata Fursa ya kuonekana katika tamasha na tutaweka jina, nembo na kiunga cha kampuni yako mbele ya maelfu ya washiriki na watazamaji, Kupitia hafla huduma zako tutazitangaza kwa hadhira yetu kupitia vipeperushi, posters, mitandao ya kijamii, redio Pamoja na Tv Channel kama Mfadhili wetu.
2. Tutakuwa na Red Carpet na Banner kubwa ambayo itakuwa na chapa ya logo mbalimbali za wadhamini wa tamasha, Kuiunganisha huduma yako na wadau mbalimbali, Siku ya hafla muwakilishi wenu atapata fursa ya kuielezea vyema huduma yako mbele ya hadhira.
MWISHO
Taasisi ya holysmile inawashukuru wadau wote wa mkoa wa shinyanga Pamoja na uongozi wa manispaa ya shinyanga kwa kuipokea taasisi ya holysmile ili kulifanikisha jambo pia amewaomba wana shinyanga kuungana katika hatua ya Upigaji kura mpaka hatua ya kuwapata washindi. Kwa maelekezo Zaidi wasiliana na uongozi kwa simu number +255 756 254 146
Wewe ni mdau shupavu holysmile tunakutambua na kukuthamini
Social Plugin