KAMATI YA BUNGE YATEMBELEA MRADI WA TASAF SHINYANGA

Kamati ya kudumu ya bunge ya utawala katiba na sheria ikitembelea mradi wa TASAF wa ufunguzi wa Barabara Mtaa wa Mwadui Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

KAMATI ya kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria imefanya ziara katika Manispaa ya Shinyanga, kwa kutembelea mradi wa ufunguzi wa barabara kilomita 2.5 ambao unatekelezwa na walengwa wa TASAF Mtaa wa Mwadui Kata ya Ngokolo kwa gharama ya Sh. milioni 25.6.

Kamati hiyo imefanya ziara leo Machi 15,2023 ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati Florent Kyombo na kuhudhuriwa pia na Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama pamoja na Naibu Waziri Paulina Gikuli na Ridhiwani Kikwete.

Kyombo akizungumza kwenye ziara hiyo, amesema fedha za TASAF zimekuwa na mchango mkubwa kuchochea maendeleo, pamoja na kuzinyanyua Kaya Maskini kiuchumi.

"Miradi hii ya TASAF ambayo imekuwa ikiibuliwa na walengwa wa TASAF ikiwamo ya ufunguzi wa barabara napenda kutoa msisitizo kwa halmashauri, barabara hizi ziboreshwe na TARURA ili ziwe za kiwango kikubwa," amesema Kyombo.

Naye Waziri Mhagama amesema Serikali chini ya Rais Samia imekuwa ikitenga fedha nyingi kwa ajili ya walengwa wa TASAF na katika Bajeti ya iliyopita kimetengwa kiasi cha Sh.bilioni 496 na kwa Mkoa wa Shinyanga zimepelekwa Sh.bilioni 51.4.

Amesema Ofisi yake itaendelea kusimamia fedha hizo za TASAF kwenye Program ya miradi ya jamii, ili maono ya Rais Samia yafikiwe na kuchochea maendeleo na kuziinua Kaya maskini kiuchumi.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, ametumia fursa hiyo kumpongeza Rais Samia kwa kuendelea kuleta fedha za miradi ya maendeleo mkoani humo zikiwamo na fedha za walengwa wa TASAF Sh.bilioni 51.14 na miradi ya TASAF kwa mkoa mzima ipo 598, huku akiahidi kusimamia miradi hiyo na matumizi sahihi ya fedha.

Nao walengwa wa TASAF akiwamo Habiba Shango, wameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa fedha hizo za TASAF ambazo zimekuwa zikiwasaidia katika maisha yao kiuchumi na kufikia hatua ya kujenga nyumba na kusomesha watoto.

Kamati hiyo ya Bunge pia imetembelea ujenzi wa Jengo la Mwendesha Mashtaka (DPP).
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria Florent Kyombo akizungumza na walengwa wa TASAF Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga.
Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama akizungumza na walengwa wa TASAF Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga.
Naibu Ofisi ya Rais Waziri Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete akizungumza na walengwa wa TASAF Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza na walengwa wa TASAF Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akizungumza na walengwa wa TASAF Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza na walengwa wa TASAF Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga.
Mlengwa wa TASAF Habiba Shango akitoa shukrani kwa Serikali kutoa fedha za TASAF na kuwainua kiuchumi.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimneti ya utumishi wa umma na utawala Bora Ridhiwani Kikwete (kulia) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme kwenye Mkutano na Walengwa wa TASAF Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga.
Afisa elimu Mkoa wa Shinyanga Dafroza Ndalichako (kushoto) akiwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi kwenye Mkutano na walengwa wa TASAF Kata ya ngokolo Manispaa ya Shinyanga.
Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria wakiwa kwenye Mkutano na walengwa wa TASAF Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga.
Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria wakiwa kwenye Mkutano na walengwa wa TASAF Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga.
Walengwa wa TASAF wakiwa kwenye Mkutano wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria.

Mkutano wa walengwa wa TASAF Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga ukiendelea na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria.

Ukaguzi wa Barabara ambayo imetengenezwa na Walengwa wa TASAF Mtaa wa Mwadui Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga.
Muonekano wa Barabara ambayo imetengenezwa na walengwa wa TASAF Mtaa wa Mwadui Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post