NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KLABU ya Simba imefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kufanikiwa kuichapa Horoya AC kwa mabao 7-0, mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa.
Simba Sc ilianza kupata bao kupitia kwa Clatous Chama ambaye alipiga mpira wa adhabu na kutinga moja kwa moja wavuni na baadae Jean Baleke akapachika bao la pili baada ya Kipa wa Horoya kuokoa shuti kali lililopigwa na Kibu Denis na kukuta Baleke na kuzamisha wavuni.
Bao la tatu limefungwa kwa njia ya penati kupitia kwa nyota wao Chama ambaye alifunga kwa mkwaju wa penati baada ya mchezaji wa Horoya kuunawa mpira na kuamlishwa penati.
Mpaka mapumziko Simba Sc ilikuwa iko mbele kwa mabao 3-0, huku kipindi cha pili wakirudi kwa kasi na kufanikiwa kupata mabao mengine kupitia kwa Baleke na kufiikisha mabao mawili kwenye mchezo huu, Chama ambaye amefunga matatu (Hat Trick) pamoja na Sadio Kanoute ambaye nae amefunga mawili.