Mwenyekiti wa Wanawake DART Mwamvua Stambuli akikabidhi moja ya Msaada kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya ikiwa ni maadhimishi ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo hufanyika Machi 8 ya Kila mwaka.
Baadhi ya picha mbalimbali ya Wanawake wa DART katika Hospitali ya Mbagala Rangi Tatu walipokwenda kutoa msaada kwenye maadhimisho ya Siku Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa kila machi 8 ya Kila Mwaka.
**************
Na Mwandishi Wetu
Wanawake wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani wametoa msaada wa vitu mbalimbali Hospitali ya Mbagala Rangi Tatu kwa kuonyesha upendo kwa wananchi katika kujali afya zao.
Akizungumza wakati wa Kukabidhi msaada huo Mwenyekiti wa Wanawake wa DART Mwamvua Stambuli amesema kuwa msaada huo ni kutokana na kutambua umhimu wananchi wa Mbagala kwani siku za usoni watakuwa wateja wa kutumia huduma za usafiri wa mabasi yao.
Amesema wanawake wa DART wameguswa kipekee na kujitoa kwa wanawake wanaojifungulia hapo kupata msaada wa mahitaji mbalimbali.
Msaada wa DART unamegharimu shilingi milioni Nane kwa kununua mashuka 40 , Baiskeli ya kubebea waginojwa , Sabunj ya vipande, sabuni ya unga , Dawa ya Mswaki, pamoja na mashine mbalimbali
Aidha amesema katika msaada waliotoa utasaidia kutatua baadhi ya changamoto kwani kama wanawake wametambua ni mahitaji wanawake ikiwemo mashuka kwa ajili ya hospitali hiyo.
Mwenyekiti huyo amesema licha ya kutoa msaada huo kwani itakuwa ndio mwendelezo kutokana na kutambua mahitaji ya hospitali hiyo.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mbagala Rangi Tatu Ally Makori ameshukuru msaada huo na kutaka baadhi ya Taasisi kuiga mfano mzuri kwa DART.
Amesema hospitali hiyo wanawake wanaojifungua katika hospitali hiyo kwa siku ni kati 30 hadi 40 hivyo msaada huo ni mkubwa kutokana na mahitaji ya wanawake hao.
Mmoja ya Mwanamke aliyejifungua katika Hospitali Asha Hamis amesema msaada huo kwao ni mkubwa kwani maadhimisho hayo yamegusa wanawake tulifika katika hospitali hiyo.
Social Plugin