Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KAMATI YA BUNGE YAPONGEZA WCF USAJILI WAAJIRI


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma (hayupo pichani) kutoa mada kuhusu utekelezaji wa majukumu ya mfuko huo kwa wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Bungeni, Jijini Dodoma

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma akiwasilisha mada kuhusu utekelezaji wa majukumu ya mfuko huo kwa wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Bungeni, Jijini Dodoma.


Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii wakifuatilia kwenye vishikwambi mada kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mfuko huo, Dkt. John Mduma (hayupo pichani), Bungeni, Jijini Dodoma.


Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe Mhe. Fatuma Toufiq wa pili kutoka (kushoto) akieleza jambo mara baada ya kupata taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mfuko huo, Dkt. John Mduma (hayupo pichani), Bungeni, Jijini Dodoma


Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Ali Hassan Omar akichangia hoja mara baada ya kupata taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mfuko huo, Dkt. John Mduma (hayupo pichani), Bungeni, Jijini Dodoma l


Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Sophia Mwakagenda akichangia hoja mara baada ya kupata uelewa wa utekelezaji wa majukumu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) iliyowasilishwa wajumbe wa kamati hiyo, Bungeni, Jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Abdulssalaam Omar akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, mara baada ya kuwasilisha mada kuhusu utekelezaji wa majukumu ya mfuko huo.



PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)



Na: Mwandishi Wetu - DODOMA

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imepongeza Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) uliopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wa kusajili waajiri kwa asilimia 92.2.

Akizungumza leo Machi 23, 2023 katika kikao cha kamati cha kupokea utekelezaji wa majukumu ya Ofisi hiyo na taasisi zake, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Fatuma Toufiq, ameupongeza mfuko kwa hatua hiyo na kuahidi kuendelea kuishauri vyema serikali.

Naye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameahidi Ofisi yake itaendelea kushirikiana na kamati hiyo ili ifanye kazi yake ya kuishauri serikali.

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya WCF, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Dk.John Mduma, amesema hadi sasa asilimia 92.2 ya waajiri wamesajiliwa.

Amesema usajili wa waajiri umeongezeka kutoka waajiri 5,178 sawa na asilimia 17.2 kwa mwaka 2015/16 hadi kufikia waajiri 27,786 sawa na asilimia 92.2 kwa mwaka 2021/22.

Aidha, amesema katika kipindi cha miaka saba ya utekelezaji wa mfuko huo umelipa fidia kiasi cha Sh.Bilioni 44 huku kiwango cha fidia kwa mwaka kimeongeza kutoka Sh.bilioni 1.5 hadi Sh.Bilioni 13.

“Mapato ya uwekezaji yameongezeka kutoa Sh.bilioni 1.6 tulivyoanza hadi kufikia mwaka 2021/22 ilifikia Sh.bilioni 74,” amesema

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com