********************
Na Mwandishi Wetu
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi ameshiriki mkutano wa Mawaziri wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika(SADC) unaojadili masuala ya kazi na ajira katika nchi hizo.
Mkutano huo umefanyika Kinshasa, Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo kuanzia Machi 27-31, 2023 ambapo Mawaziri hao wamepeana uzoefu kuhusu namna baadhi ya nchi zinavyopambana kutatua changamoto za ajira.
Aidha, Mawaziri hao wamepata fursa ya kutembelea Chuo kinachofundisha masuala ya kazi na ajira (VETA) nchini Kongo ili kujionea namna chuo hicho kinavyotoa mafunzo kwa vijana kwa lengo la kupunguza tatizo la ajira nchini humo
Social Plugin