WAZIRI wa Madini nchini Dotto Biteko,amemtambulisha Katibu mkuu wa Wizara hiyo Kheri Mahimbali, kwa watumishi wa idara zote za wizara ya madini huku akimkabidhi majukumu matatu ya kuyafanyia kazi.
Akiongea kwenye kikao cha utambulisho leo March 10,2023 Jijini Dodoma, Waziri Biteko amemtaka katibu Mkuu huyo aliyeteuliwa hivi karibuni na Rais Samia Suluhu Hassan kuishi kwa kuimarisha utendaji wa watumishi ili wafanye kazi kwa bidii.
Miongoni mwa mambo ambayo Waziri huyo ametaka kuzingatia ni pamoja na kusimamia malengo ambayo wizara hiyo imekabidhiwa na serikali kuyafanyia kazi ili yakamilike kwa wakati.
"Katika wizara hii wapo watu wa aina mbalimbali ambao utakwenda kufanya nao kazi hivyo unapaswa kuwa makini ili kuhakikisha kazi zinafanyika na kufikia malengo ya serikali kama ambavyo yamepangwa;
Nikwambie tu hapa unaowaona watu wa kila aina,wapo ambao ukiwapa kazi wao wanaangalia ‘dead line’ hata kama kazi uliwapa haijakamilika wanakuletea, lakini wapo ambao kazi hawamalizi kwa wakati na wala majibu hawakupi,
Vilevile wapo ambao wao kazi hawafanyi kabisa, lakini wapo wengine ambao wao ukiwapa kazi wanafanya na ukiwarekebisha wanafurahi kurekebishwa "amesema Biteko
Pamoja na mambo mengine amesema kutokana na muda mwingi watumishi kuutumia wakiwa kazini katibu mkuu anatakiwa kuwafanya waajria kujiona wao ni wa muhimu katika wizara hiyo.
"Ili ufaulu vizuri hakikisha unamfanya mtumishi ambaye hataki kufanya kazi yake aifanye na kuipenda, mbinu gani utatumia unazijua vizuri mimi sitaki kukufundisha,"amesema
Aidha katika jambo la tatu Waziri Biteko alimtaka Katibu mkuu huyo kuiweka Wizara hiyo kuwa kioo Kwa Kila mtu na kumfanya kila mtanzania atamani kufanya kazi kwenye Wizara ya madini.
Kutokana na hayo Naibu waziri wa Madini Dk. Steven Kiruswa, amesema yapo mambo mengi ambayo wameyafanyia kazi hadi sasa ikiwemo kupunguza idadi ya watu waliokuwa wamekaimu katika nafasi mbalimbali ndani ya wizara hiyo.
"Katibu mkuu nashukuru kuwa umeeleza kuwa unapaenda kufanya kazi kama timu mie pia ni muumini wa ushirikishwaji lakini tangu nimeingia madarakani katika nafasi hii ni mwaka mmoja na miezi kadhaa mambo mengi tumeyafanyia kazi ikiwemo kupunguza idadi ya watu walikua wakikaimu katika nafasi mbalimbali,"amesema
Social Plugin