Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAAFISA MAWASILIANO NA UHUSIANO SERIKALINI WAASWA KUTANGAZA MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI WA MKUMBI


Kaimu Mkurugenzi Kitengo cha Mazingira ya Biashara cha Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Bw. Baraka Aligaesha amewashauri Maafisa Mawasiliano na Uhusiano Serikalini kutangaza na kielimisha umma kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji nchini (MKUMBI) .

Bw. Baraka ameyasema hayo wakati akiwasilisha mada kuhusu utekelezaji wa MKUMBI na mafanikio yake katika Kikao Kazi cha 18 cha Maafisa Mawasiliano na Uhusiano Serikalini (TAGCO) Machi 29, 2023 JNICC jijini Dar es Salaam

Akiongea na Maafisa hao, amesema ni jukumu la kila Afisa Mawasiliano na Uhusiano Serikalini kutangaza na kuelimisha umma kuhusu maboresho yanayotokea katika sekta husika kutokana na utekelezaji wa MKUMBI ili kuvutia wawekezaji na kuwahamasisha ufanyaji biashara nchini

Akifafanua kuhusu mafanikio hayo amesema Serikali kwa kishirikiana na Sekta Binafsi imefanikiwa kurekebisha sheria 42 kati ya 88 zilizokuwa kero, kufuta ada, faini na tozo 232 kati ya 380 na

Mafanikio memgine aliyoyataja ni kuunganisha au kuondoa majukumu yanayofanana kwenye mamlaka za udhibiti ili kurahisisha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa sekta binafsi kama vile majukumu ya udhibiti wa chakula na vipodozi yaliondolewa TFDA na kuhamishiwa TBS na hivyo kuanzishwa kwa TMDA.

Vilevile amesema Serikali imefanikiwa kuanzisha Mifumo ya TEHAMA ambayo imesaidia kupungua kwa muda wa usajili wa hospitali binafsi kutoka miezi 12 hadi miezi 3, muda wa usafirishaji wa mizigo kutoka Dar es salaam hadi mpaka wa Tunduma kutoka siku 7 hadi 3, muda wa kupata cheti cha usajili wa sehemu za kazi kutoka siku 14 hadi siku 1, muda wa kutoa leseni ya OSHA kutoka siku 28 hadi siku 3; na muda wa kushughulikia maombi ya vibali vya kazi kutoka siku 14 hadi kati ya siku 3 hadi 7.

Bw Baraka pia amesema MKUMBI imefanikiwa kuanzisha Mfumo wa Tehama wa Huduma za Pamoja kwa Wawekezaji unaolenga kuunganisha mifumo ya Taasisi 12 zinazotoa Huduma chini ya TIC ambazo ni TIC, NIDA, TRA, BRELA, Idara ya Kazi, Uhamiaji, Ardhi, TBS, TMDA, NEMC, TANESCO na OSHA ili kumuwezesha Mwekezaji kupata vibali vya uwekezaji kwa urahisi ma gharama nafuu.

Aidha, amesema Idara ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji zimeanzishwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kuchochea kasi ya uboreshaji wa mazingira ya biashara na kuhudumia sekta binafsi na kutatua changamoto zao kwa haraka pamoja na Uanzishaji wa Kitengo cha Uratibu wa MKUMBI chenye majukumu ya kufuatilia utekelezaji wa shughuli kwa mujibu wa mpango wa utekelezaji wa maboresho.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com