SOUWASA YASAINI MKATABA UJENZI WA MRADI MKUBWA WA MAJI SONGEA


Katibu Mkuu Wizara ya Maji akisaini mkataba na mkandarasi wa China Civil engineering Construction Corporation (CCECC) mjini Songea Machi 10, 2023
Mkuu wa mkoa Ruvuma Kanal Laban Thomas akiongea kwenye hafla ya utiaji Saini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji manispaa ya Songea
Balozi wa Maji Mrisho Mpoto akitumbuiza 
Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Marry Prisca Mahundi akiongea wakati wa hafla ya kutia Saini mradi mkubwa wa Maji mjini Songea
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira manispaa ya songea (SOUWASA) Mhandisi Patrick Kibasa
Baadhi ya Wananchi wakishudia Wizara ya Maji wakisaini mkataba wa Maji Kwenye viwanja vya Shule ya msingi Matarawe mjini Songea

***

Na Andrew Chatwanga ,Songea

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Songea SOUWASA Mhandisi Patrick Kibasa amesema mamlaka yake kwa sasa ina uwezo wa kusambaza maji lita milioni 11.58 kati ya Lita  milioni 20.33 zinazohitajika kwa siku.


Mhandisi Kibasa aliyasema hayo Machi 10,2023 wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa miji 28 katika mji wa Songea wenye thamani ya Tsh Bilioni 145.7.7 kati ya wizara ya maji na mkandarasi wa China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) kwenye viwanja vya Shule ya msingi Matarawe.


Awali Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba alisema mradi huo utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kuhudumia wakazi wa Manispaa ya Songea hadi mwaka 2045.


Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Marry Prisca Mahundi alisema mradi huo utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kuzalisha maji lita Milioni 31 kwa siku na kuwa na ziada ya Lita zaidi ya Milioni 8 kwa siku.

Naibu Waziri Mahundi aliwataka wakazi wa Songea kutunza mazingira hasa kwenye vyanzo vya maji ili miradi ya maji inayotekelezwa na Serikali iwe endelevu na kuwa na manufaa makubwa kwa kizazi cha sasa na kijacho.


Mkuu wa mkoa Ruvuma Kanal Laban Thomas alisema mkoa wake unatekekeza miradi ya maji kwenye wilaya za Nyasa,Namtumbo na Tunduru wenye jumla ya Tshs Bilioni 50 na amemtaka mkandarasi wa mrati wa Manispaa ya songea ambaye mkataba wake ni miezi 34 kuhakikisha anaukamilisha kwa wakati.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post