Mashindano ya mpira wa miguu ya Mkenda Cup yamezinduliwa rasmi wilaya Rombo,kwa mara ya kwanza yakishirikisha timu 91 kutoka kata mbalimbali za wilaya hiyo.
Mashindano hayo ambayo yamezinduliwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Patrick Boisafi katika uwanja wa Sabasaba na yamedhaminiwa na Mbunge wa jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda na Wadau.
Kwa mujibu wa Prof.Mkenda mshindi wa kwanza wa michuano hiyo ataibuka na kitita cha shilingi milioni tatu pamoja na ziara ya kutembelea Makao Makuu ya nchi,mshindi wa pili atapata shilingi milioni 2 na wa tatu atapata milioni moja.
Katika mechi ya ufunguzi wa michuano hiyo mabingwa watetezi timu ya Rongai Fc waliwafunga Motamburu Kitendeni Fc kwa penati 5-4 baada ya kutoka sare ya nao 1-1 katika muda wa dakika tisini na kufanikiwa kupata zawadi ya mbuzi mnyama.
Social Plugin