Mshauri Mwandamizi wa Rais wa Vyombo vya Habari na Uhusiano wa Umma, John Nagenda amefariki dunia.
Nagenda, mwandishi wa habari mkongwe amefariki dunia Jumamosi alasiri katika Hospitali ya Kimataifa ya Medipal mjini Kampala ambako alikuwa amelazwa kwa wiki kadhaa,taarifa zinasema kuwa alikuwa na umri wa miaka 84.
Naibu Katibu wa Habari wa Rais Museveni, Faruk Kirunda amesema kwamba Nagenda alikuwa amelazwa hospitalini kwa miezi mitatu.
Nagenda ambaye aliishi Uingereza kwa zaidi ya miaka 10 kabla ya kurejea Uganda amekuwa mwandishi wa habari wa magazeti tangu miaka ya 1960.
Social Plugin