Mnyama Fisi
Kwa mujibu wa wakazi, waliamkia mabaki ya mwili uliokuwa umevamiwa na wanyama hao huku mzoga tu ukibaki.
Tukio hilo lilifanyika kijiji cha Canaan, Mastore Juja Ijumaa Machi 3,2023 kwani wakazi walipata mabaki hayo Jumamosi.
"Umepatikana katika kichaka kilicho eneo hili lakini bado haujatambulika," mkazi aliyeshuhudia alisema.
Eneo hilo hujulikana kwa kuwa na wanyama hao ambao hutishia wakazi pakubwa kutokana na mashambulizi yake.
Aidha baadhi walisema haijabainika iwapo mauaji yalitekelezwa kwa mwathiriwa kabla ya mwili wake kutupwa ili uliwe na wanyama hao hatari.
Social Plugin