Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ikiongozwa Mwenyekiyti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka wakitembelea mradi wa ujenzi wa BRT awamu ya tatu unaotoka Gerezani-Gongo la Mboto leo Machi 29,2023 Jijini Dar es Salaam.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ikiongozwa Mwenyekiyti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka wakitembelea karakana inayotumiwa na mradi wa ujenzi wa BRT awamu ya tatu unaotoka Gerezani-Gongo la Mboto leo Machi 29,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa BRT awamu ya tatu unaotoka Gerezani-Gongo la Mboto leo Machi 29,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Rogatus Mativila akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kutembelea mradi wa ujenzi wa BRT awamu ya tatu unaotoka Gerezani-Gongo la Mboto leo Machi 29,2023 Jijini Dar es Salaam
**************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wameishauri Serikali kupitia kuangalia uwezekano wa kufanya maboresha katika eneo la daraja la Mfugale TAZARA kwenye makutano ya barabara ili kuondokana na msongamano mkubwa wa magari pindi mradi wa mabasi yaendayo haraka utakapo kamilika..
Ushauri huo umetolewa leo Machi 29,2023 Jijini Dar es Salaam, Wakati Kamati hiyo ikiongozwa na Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka ikishirikiana na Ofisi ya Taifa ya ukaguzi wa Hesabu za Serikali kufanya ziara ya kutembelea miradi wa ujenzi wa mabasi yaendayo haraka BRT III Gerezani-Gongo la Mboto.
Amesema wamewashauri waangalie wanatatua vipi tatizo hilo ili kuondoa usumbufu utakaojitokeza pindi mradi huo utakapokamilika na kuanza kutumika.
"Hili kama halijaangaliwa, suala la kuwa na mabasi yaendayo kasi inaweza ikawa haina maana kwamaana kutakuwa na msongamano wa magari mengi na ukizingatia ndo njia ya magari makubwa (maroli) yanayotoka bandarini yanapita hapo". Amesema
Aidha amesema katika eneo lingine ambalo waliangali ni pamoja na sehemu ya kujenga karakana ya BRT III imekuwa na matatizo mengi, wamekuwa wakipata eneo na kuanza shughuli zao na kuondolewa kwa sababu zisizo za msingi na kufanya kutafuta eneo lingine wakati fedha zimeshatumika katika uandaaji wa karakana eneo hilo.
"Wameenda Killtex wameanza kutengeneza.....wanaambiwa hapana hapa ni kwa mwekezaji mbinafsi, mwekezaji mmoja azuie kazi ambayo imeshaanza ya kutengeneza karakana alafu ihamishwe kwa vile kuna mwekezaji, lakini miaka yote mwekezaji hajafanya lolote, kwahiyo ukiangalia hapa kuna mchezo mchafu unafanyika". Amesema
Amesema miradi inapoanza lazima ipangwe vizuri ili kuoondokana na changamoto ambazo mwisho inaleta changamoto ya kulipa fedha nyingi pasipo sababu na miradi inashindwa kuendelea bila sababu maalumu.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Rogatus Mativila amesema mpaka sasa mkandarasi yupo kwenye asilimia 5% na alikuwa anatakiwa kuwa katika asilimia 15% hivyo mkandarasi huyo ameahidi kuhakikisha anaziba gepu la asilimia hizo kwa kufanya kazi kwa bidii usiku na mchana pamoja na kuongeza wafanyakazi.
Pamoja na hayo ameipongeza kamati kwa kuwasaidia kuwapamaelekezo mbalimbali mazuri ambayo yanawasaidia katika utekelezaji.
"Maelekezo ambayo yametolewa na kamati tumeyachukua ambapo tutaenda kuyatekeleza ikiwemo utaratibu wa kupunguza msongamano kwenye daraja la Mfugale pale TAZARA". Amesema.
Social Plugin