KAIMU Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Dkt.Charles Mhina,akizungumza wakati wa Kikao cha Mashirikiano ya Sekta ya Mifugo kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ( SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kilichofanyika leo Machi 3,2023 jijini Dodoma.
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo,Umwagiliaji,Maliasili na Mifugo Zanzibar, Bw.Omar Ali Amir ,,akizungumza wakati wa Kikao cha Mashirikiano ya Sekta ya Mifugo kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ( SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kilichofanyika leo Machi 3,2023 jijini Dodoma.
SEHEMU ya Washiriki wakifatilia hotuba ya Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Dkt.Charles Mhina, wakati wa Kikao cha Mashirikiano ya Sekta ya Mifugo kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ( SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kilichofanyika leo Machi 3,2023 jijini Dodoma.
KAIMU Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Dkt.Charles Mhina,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya Kikao cha Mashirikiano ya Sekta ya Mifugo kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ( SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kilichofanyika leo Machi 3,2023 jijini Dodoma.
Na.Erick Mungele-DODOMA
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ( SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) zaimarisha ushirikiano Ili kutatua changamoto kwenye Sekta ya Mifugo ili kufikia uzalishaji wenye tija zaidi.
Akizungumza leo Machi 3,2023 jijini Dodoma Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Dkt.Charles Mhina,wakati wa Kikao cha Mashirikiano ya Sekta ya Mifugo kati ya SMT na SMZ.
Dk, Mhina amesema lengo la ushirikiano huo ni kuimarisha na kuondoa vikwazo vilivyopo katika kuiendeleza sekta ya mifugo nchini.
‘’Tumekuwa tukishirikiana pia kwenye maeneo ya masoko kuona ni namna gani tunaweza tukaimarisha masoko ya bidhaa za mifugo kwa pande zote mbili. Kwa hiyo ushirikiano huu unalenga kuondoa vikwazo ambavyo vinaweza kuifanya biashara ya mifugo isikue kwa haraka ,’’ amesema Dkt. Mhina
Aidha Dkt. Mhina amesema kuwa sehemu zote za Bara na Zanzibar kuna viwanda vya kuzalisha bidhaa za mifugo ikiwemo nyama, ngozi, maziwa na bidhaa nyingine hivyo ushirikiano huo utasaidia kuimarisha sekta hiyo ya mifugo.
''Niwaombe wajumbe wajikite zaidi kujadili changamoto na kuzitafutia majibu na kisiwe kikao cha kuzalisha changamoto maana itasaidia kujua wapo saihihi au bado katika kufika malengo ya uzalishaji wa tija''amesema Dkt.Mhina
Amesema kupitia kikao hicho mkulima wa kawaida yaani mfugaji itamsaidia kupitia tafiti kumshauri kutumia mbegu gani na kuzalisha zaidi na kutumia mitambo sahihi na inayozalishwa hapa Tanzania.
Hata hivyo ameongeza kuwa ushirikiano huo umelenga kutatua changamoto kwenye maeneo mbalimbali hususan changamoto za kikodi kwa kushauri mamlaka husika ziweze kufanya marekebisho ili kuwezesha biashara kufanyika kwa urahisi zaidi kati ya pande zote mbili za muungano.
"Lakini ushirikiano huu pia utatuwezesha kutumia fursa za pamoja kama zitakuwepo ikiwemo fursa za kusafirisha bidhaa za nyama kwenda nje ya nchi ili tuweze kuyafikia masoko hayo kwa kiasi kikubwa,’’ amefafanua Dkt. Mhina.
Aidha, alibainisha kuwa ushirikiano huo utajikita pia katika maeneo ya utafiti na mafunzo ili waweze kujifunza kila upande ni namna gani sekta zinafanya ili kuzalisha kwa tija mifugo na bidhaa zake.
‘’Pia tutajifunza ni kwa namna ganina wafugaji wa sekta binafsi wanawezeshwa kutumia fursa zilizopo kuzalisha kwa tija na kuongeza mchango wa sekta ya mifugo katika pato la taifa,’’ ameeleza
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo,Umwagiliaji,Maliasili na Mifugo Zanzibar, Bw.Omar Ali Amir ,amesema kuwa wanatumia ushirikiano huo kujifunza tafiti mbalimbali na pia kujenga uwezo wa wataalam wao kupitia Tanzania bara kwa maana Tanzania bara wako mbele kwenye masuala mbalimbali ikiwemo uzalishaji, Masoko, na Utafiti.
‘’Sekta ya mifugo sio ya muungano, lakini ni sekta ambayo inahitaji ushirikiano, mfano wafugaji wanaposafirisha mifugo kutoka eneo moja kwenda jingine kunakuwa na changamoto za kisera ,kisheria hivyo kupitia ushirikiano huu changamoto nyingi tunaweza kuzimaliza kwa ustawi wa pande zote mbili,’’ amesema Dkt.Amir
Social Plugin