Mkuu wa Chuo Cha Ustawi wa Jamii (ISW), Dkt. Joyce Nyoni akifungua Mafunzo kwa mabinti wanyakazi wa ndani 100 leo Machi 18,2023 katika ukumbi wa Chuo hicho Jijini Dar es Salaam
***************
Chuo cha Ustawi wa Jamii (ISW) leo Machi 18 kimetoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa malezi na makuzi ya watoto zaidi ya kwa wasichana 100 ambao wanyafanya kazi za ndani katika Mkoa wa Dar Es Salaam.
CHUO cha Ustawi wa jamii (ISW) kimefanikiwa kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa malezi na makuzu ya watoto Wasichana wanaofanya kazi za ndani 100 katika Mkoa wa Dar es Salaam ili kupunguza ama kuondoa changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabiri wasicchana hao na nyumba ambazo wanafanyia kazi.
Akizungumza na Waandishi wa habari Leo Machi 18,2023 Jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mafunzo hayo Mkuu wa Chuo hicho ,Dkt. Joyce Nyoni amesema awali tulikuwa tunajaribu kuona muititikio wa wadada kuja katika mafunzo haya lakini maombi yaliyotufikia ni zaidi ya 200 hivyo watafanya mafunzo hayo zaidi siku zijazo.
“Leo tuna programu ya kuwajengea uwezo wadada wakazi katika malezi na makuzi ya mtoto tumeifanya hili tukiwa tunaelekea kuadhimisha siku ya ustawi wa Jamii Machi 21". Amesema
Dk Nyoni ameeleza kuwa hivi karibuni kumekuwa na kelele nyingi na malalamiko kuhusu malezi na tabia za watoto kwahiyo wakaona kama mchango wao wawe na vipindi na wasaidizi hao ambao wanalea watoto nyumbani kwasababu wanakaa na watoto muda mrefu.
Amesema akinamama wengi wanaondoka asubuhi na kurudi jioni na mtoto anakaa na dada lakini dada hana uelewa kuhusu malezi na makuzi na ana mchango mkubwa katika kulea.
“Lakini tunatambua dada huyu kuna siku atakuwa mama ni muhimu kuelewa ni namna gani anapaswa kulea mtoto kutokana na mabadiliko tunamjenge uwezo wa kumuelewa mtoto na kuwa na msaada chanya katika maendeleo na makuzi ya mtoto,”amesisitiza.
Amebainisha kuwa baada ya kutoa tangazo hilo Watu wanaokaa na wadada wakazi wengi walisema wanakuja kuwahamasisha kupata haki zao ambapo dhana hiyo inamaanisha kuwa hawakai nao vizuri.
“Niwasihii sana hawa ni wale ambao tunawaachia watoto tukae nao vizuri hakuna binadamu ambaye hana mapungufu aelekezwe vizuri kwasababu ndio tunawaachia watoto jinsi unavyokaa naye vibaya anaweza kuhamishia kwa watoto wananafasi kubwa sana katika malezi na makuzi ya watoto,”ameeleza.
Aidha ameeleza kuwa Wakati mwingine ukatili unatokea kwasababu dada hamuelewi mtoto kama dada atamuelewa anatajua namna yakumsaidia na mama pia anatakiwa kumsaidia dada awe katika mazingira ya kujiamini anavyomlea mtoto .
Mmoja wa wafanya kazi wa ndani kutoka Bunguruni alisema mafunzo haya yanawajenga uwezo kwani wanafundishwa vitu wanavyotakiwa kujua pia kama wazazi wa baadae .
“Mfano tumefundishwa kuhusu ukuaji wa mtoto kimwili,kiakili ,kiroho na kijamii mafunzo yanatujenga tujue je zile hatua na ukuaji anaopitia mtoto ni sawasawa na vile tumeeelekezwa kama kuna changamotu turipoti kwa mama.
Alieleza kuwa Changamoto wanazokutana nazo ni mahusiano ya mtoto na mama kwani muda mwingine mama anakuwa bize hapati muda wakuongea naye kuhusu mtoto anapitia changamoto gani, mama akirudi anakuwa bize na simu au anaenda chumbani kulala .
“Muda mwingine ukimwabia nataka kuongea na wewe anakwambia amechoka kesho na kesho ikifika umejisahau na ukitaka kumwambia yuko bize unakuwa na ugumu wa kumwabi na wakati mwingine hayupo makini na kile ambacho nataka kumwambia ,”alibainisha. Wahadhiri wa Chuo hicho wametoa pia mafunzo ya Jinsi ya kukabiliana na misongo ya mawazo, matumizi sahihi ya fedha na kuweka akiba, usafi na mawasiliano kwa Wadada hao.