Na Mwandishi Wetu,UNESCO- NEW YORK
Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amekutana na Naibu Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa UNESCO Bwana Xing Qu ofisi za UNESCO New York kwa lengo la kujadiliana juu ya mahusiano na mashairikiano katika usimamizi wa uendelezani wa Rasilimali za Maji na ushirikiano katika usimamizi wa Maji Shirikishi.
Waziri Aweso amewasilisha ombi la Tanzania kujengewa uwezo na UNESCO katika usimamizi na uendelezaji wa Rasilimali za Maji na utekelezaji wa miradi ya Maji, uandaaji wa maandiko ya Miradi na utafutaji wa fedha.
Aidha; Naye Naibu Mkurugenzi mkuu UNESCO Mr Xing Qu ameahidi ushirikiano katika maeneo ya kipaumbele kwa Afrika ikiwemo usimamizi wa Maji chini ya Ardhi, kujenga uwezo wa taasisi katika tathmini ya usimamizi wa Rasilimali za Maji.