Meneja wa Fedha TGNP Bw.Altho Mwangoa akizungumza katika Kilinge salama maalumu cha wanaume kugusia masuala ya Nafasi ya wanaume katika kuendeleza usawa wa kijinsia kilichofanyika leo Machi 25,2023 kwenye ukumbi wa Lost Beach Jijini Dar es Salaam.
********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Lengo la usawa wa kijinsia katika Nyanja zote ni kwaajili ya kuboresha hali za kiuchumi, kuhimiza ustahimilivu, kuleta haki kwa kila mmoja (hasa haki ya kuishi) mwisho wa siku kujenga taifa lililo bora.
Ameyasema hayo leo Machi 25,2023 Jijini Dar es Salaam, Meneja wa Fedha TGNP Bw.Altho Mwangoa wakati akifungua Kilinge salama maalumu cha wanaume kugusia masuala ya Nafasi ya wanaume katika kuendeleza usawa wa kijinsia .
Amesema kuwa dhana ya wanaume kufunguka kulingana na mila na desturi kunamaanisha udhaifu na fedheha lakini, unapowaweka wanaume pamoja katika kundi, wanajiamini zaidi, wanazungumza akili zao, na wanapatikana kihisia.
"Jamii imewafundisha wanaume ''man up'' na kukabiliana na mapambano yao. Hata hivyo, wakati kuna nafasi salama ambapo wanaweza kuzungumza juu ya siri zao za giza, matamanio ya kujificha, au mawazo yao juu ya uanaume (masculinity), hubadilisha maoni yao juu ya hisia na ufanyaji maamuzi". Amesema.
Pamoja na hayo amesema takwimu mbalimbali zinaonesha kuwa bado kuna pengo kubwa la wanawake katika sekta ya teknolojia nchini, na kulingana na takwimu za GSMA Intelligence, Tanzania inapengo la kijinsia kwa asilimia 11 ambapo wanawake (asilimia 77) na wanaume (asilimia 86).
Kwa upande wa washiriki wameipongeza TGNP kwa kuwapa nafasi kushiriki kongamano hilo kwani wameweza kupata uelewa kuhusu sheria za kutumia mitandao ya kijamii pamoja na madhara yatakayojitokeza pindi udhalilishaji kwa wanawake utakapojitokeza.
Bw.Benard Mwakyembe ambaye ni mmoja wa washiriki amesema amejifunza jinsi ya kupambana na ukatili wa kijinsia mitandaoni hivyo ameshauri makongamano kama haya yafanyike kuanzia ngazi ya vijiji, mitaa, kata, pamoja na wilaya ili kutoa mafunzo zaidi kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia na jamii ipate uelewa mkubwa na kutokomeza vitendo hivyo.
"Tuwe huru kwenye mahisiano yetu kuhusu hizi simu za smartphones kwani tukiwa wazi hatutaweza kuweka contents za kuwadhalilisha wamama na mabinti zetu mitandaoni". Amesema mmoja wa washiriki wa Kongamano hilo.
Meneja wa Fedha TGNP Bw.Altho Mwangoa akifungua Kilinge salama maalumu cha wanaume kugusia masuala ya Nafasi ya wanaume katika kuendeleza usawa wa kijinsia kilichofanyika leo Machi 25,2023 kwenye ukumbi wa Lost Beach Jijini Dar es Salaam. Mwezeshaji Adv.Pasiense Mlowe akizungumza katika Kilinge salama maalumu cha wanaume kugusia masuala ya Nafasi ya wanaume katika kuendeleza usawa wa kijinsia kilichofanyika leo Machi 25,2023 kwenye ukumbi wa Lost Beach Jijini Dar es Salaam. Mwezeshaji Dkt.Kitanta Simwanza akizungumza katika Kilinge salama maalumu cha wanaume kugusia masuala ya Nafasi ya wanaume katika kuendeleza usawa wa kijinsia kilichofanyika leo Machi 25,2023 kwenye ukumbi wa Lost Beach Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wanaume wakifuatilia Kilinge salama maalumu cha wanaume kugusia masuala ya Nafasi ya wanaume katika kuendeleza usawa wa kijinsia kilichofanyika leo Machi 25,2023 kwenye ukumbi wa Lost Beach Jijini Dar es Salaam.
Social Plugin