Mwezeshaji kutoka TGNP, Bw.Deogratius Temba wakati akiwasilisha rasimu ya Sera ya Jinsia ya Chama cha CHAUMMA mbele ya Kamati Kuu ya Chama hicho leo Machi 11, 2023 katika ofisi za Chama hicho Jijini Dar es Salaam. Mwezeshaji kutoka TGNP, Bw.Deogratius Temba wakati akiwasilisha rasimu ya Sera ya Jinsia ya Chama cha CHAUMMA mbele ya Kamati Kuu ya Chama hicho leo Machi 11, 2023 katika ofisi za Chama hicho Jijini Dar es Salaam.
*********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KUTOKANA na Changamoto ya Ushiriki wa Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu kwenye siasa hasa kwenye nafasi za uongozi na maamuzi ndani ya vyama vya siasa TGNP iliona ni muhimu mkubwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuviwezesha vyama kutengeneza sera ya jinsia, na moja ya Chama ambacho kilinufaika kwa mara ya kwanza ni Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA).
Ameyasema hayo leo Machi 11,2023 Jijini Dar es Salaam, Mwezeshaji kutoka TGNP, Bw.Deogratius Temba wakati akiwasilisha rasimu ya Sera ya Jinsia ya Chama cha CHAUMMA mbele ya Kamati Kuu ya Chama hicho ili baadae kiweze kupeleka rasmi hiyo katika Mkutano Mkuu wa Chama hicho.
Akiwasilisha rasimu hiyo Bw.Temba amesema rasmi ya Sera ya Jinisia kwa CHAUMMA inakwenda kusaidia kukua kwa dhana ya demokraisia ya Kijamii kwa sababu wanawake, vijana, wazee na watu wenye ulemavu watapata fursa sawa ndani na nje ya chama hicho hasa katika masuala ya maamuzi.
Amesema katika mikakati ya sera hiyo, inaenda kuboresha dhana ya “Ubwabwa wa maharagwe” ili kuwa na Jamii yenye ustawi kwa kuboresha huduma za jamii hasa afya, ustawi, elimu na maji safi na salama.
"Wakati nawasilisha rasmi hii, CHAUMMA wametoa mapendekezo machache ya kuboresha lakini wameipenda kwani inaonesha na kutafsiri vizuri falsa yao ya Ubwawa na Maharage mashuleni". Amesema
Pamoja na hayo Bw.Temba amesema kuwa katika misingi ya Chama hicho, katika Katiba yake (2015), na Kanuni za uendeshaji toleo la 2012, kimebainisha misingi ya itikadi yake kuwa binadamu wote sawa, binadamu wanastahili kuwa huru na kulinda utu wao bila kukandamizwa na mtu yeyote kwa misingi rangi, kabila na jinsia.
Ameeleza kuwa dhumuni ya hii sera ni kuhakikisha wanawake wanashiriki kikamilifu kwenye nafasi za uongozi wa kisiasa na maamuzi ili kuweza kuonesha ujuzi wao katika uongozi licha ya baadhi ya jamii kuamini wanawake hawawezi katika uongozi na kufanya maamuzi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CHAUMMA Hashim Rungwe amesema wamependezwa na uwasilishwaji wa rasimu ya sera ya Jinsia ya Chama hicho hivyo basi watahakikisha sera hiyo inatekelezwa ndani ya chama na wataanza kutafuta rasilimali fedha kwaajili ya kutekeleza sera hiyo.
Kamati Kuu ya Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kikiongozwa na Mwenyekiti wao Hashim Rungwe wakimsikiliza Mwezeshaji kutoka TGNP, Bw.Deogratius Temba (hayupo pichani) wakati akiwasilisha rasimu ya Sera ya Jinsia ya Chama cha CHAUMMA leo Machi 11, 2023 katika ofisi za Chama hicho Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Hashim Rungwe akipendekez jambo mara baada ya Mwezeshaji kutoka TGNP, Bw.Deogratius Temba (hayupo pichani) kuwasilisha rasimu ya Sera ya Jinsia ya Chama cha CHAUMMA leo Machi 11, 2023 katika ofisi za Chama hicho Jijini Dar es Salaam.Kamati Kuu ya Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kikiongozwa na Mwenyekiti wao Hashim Rungwe wakipata picha ya pamoja na Mwezeshaji kutoka TGNP, Bw.Deogratius Temba mara baada ya kumisikiliza akiwasilisha rasimu ya Sera ya Jinsia ya chama hicho leo Machi 11, 2023 katika ofisi za CHAUMMA Jijini Dar es Salaam.Kamati Kuu ya Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kikiongozwa na Mwenyekiti wao Hashim Rungwe wakipata picha ya pamoja baada ya kusikiliza uwasilishwaji wa rasimu ya Sera ya Jinsia ya Chama hicho kutoka kwa Mwezeshaji wa TGNP, Bw.Deogratius Temba mara baada ya kumisikiliza akiwasilisha rasimu ya Sera ya Jinsia ya chama hicho leo Machi 11, 2023 katika ofisi za CHAUMMA Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
Social Plugin