WADAU WA MASUALA YA MAAFA WAJA NA MIKAKATI MADHUBITI YA KUDHIBITI MAAFA


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Charles Msangi akihutubia wakati wa kikao kazi cha Jukwaa la Taifa la Wadau wa Usimamizi wa Maafa kujadili rasimu ya taarifa ya tathmini na mapendekezo ya mahitaji ya mfumo wa mawasiliano ya usimamizi wa maafa na kuimarisha uelewa wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 6 ya mwaka 2022 kilichofanyika ukumbi wa hoteli ya African Dream Jijini Dodoma tarehe 7 Machi, 2023.

Afisa Sheria Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Nelson Hutty akiwasilisha mada kuhusu Sheria yaUsimamizi wa Maafa Na. 6 ya Mwaka 2022 wakati wa kikao hicho Jijini Dodoma.

Mshauri Elekezi kutoka UNICEF Bw.Sadick Masombe akitoa wasilisho wakati wa kikao kazi cha Jukwaa la Taifa la Wadau wa Usimamizi wa Maafa kujadili rasimu ya taarifa ya tathmini na mapendekezo ya mahitaji ya mfumo wa mawasiliano ya usimamizi wa maafa na kuimarisha uelewa wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 6 ya mwaka 2022

Washiriki kikao kazi cha Jukwaa la Taifa la Wadau wa Usimamizi wa Maafa kujadili rasimu ya taarifa ya tathmini na mapendekezo ya mahitaji ya mfumo wa mawasiliano ya usimamizi wa maafa na kuimarisha uelewa wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 6 ya mwaka 2022 wakifuatilia kikao hiho. Mratibu Maafa UNICEF Bi.Judith akiwasilisha mada wakati wa kikao kazi cha Jukwaa la Taifa la Wadau wa Usimamizi wa Maafa kujadili rasimu ya taarifa ya tathmini na mapendekezo ya mahitaji ya mfumo wa mawasiliano ya usimamizi wa maafa na kuimarisha uelewa wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 6 ya mwaka 2022

Afisa TEHAMA kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Givens Mtweve akiuliza swali waaati wa kikao hicho.

Naibu Kamishna Jeshi la Zima Moto na Uokoaji, Charo Mangare akifafanua jambo wakati wa kikao hicho.

Washiriki kikao kazi cha Jukwaa la Taifa la Wadau wa Usimamizi wa Maafa kujadili rasimu ya taarifa ya tathmini na mapendekezo ya mahitaji ya mfumo wa mawasiliano ya usimamizi wa maafa na kuimarisha uelewa wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 6 ya mwaka 2022 wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi rasmi.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

**************************

NA.MWANDISHI WETU

DODOMA

SERIKALI kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Menejimenti ya Maafa imedhamiria kuwa na mikakati madhubuti katika kukabiliana na maafa nchini.

Akizungumza wakati wa kikao kazi cha Jukwaa la Taifa la Wadau wa Usimamizi wa Maafa kujadili rasimu ya taarifa ya tathmini na mapendekezo ya mahitaji ya mfumo wa mawasiliano ya usimamizi wa maafa na kuimarisha uelewa wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 6 ya mwaka 2022 Kaimu Mkurugenzi wa Idara hiyo Bw. Charles Msangi alisema Idara imeendelea kuchukua hatua za kupunguza madhara kwa kuhakikisha usimamizi na uratibu wa maafa na huduma za dharura zinatolewa kwa wakati.

Kikao kazi hicho kilichoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) ilifanya Tathmini ya Mahitaji ya Mfumo wa Usimamizi wa Maafa (Disaster Management Information System Requirement mapping) ambapo rasimu ya taarifa ya tathmini ya mahitaji (Needs assessment and proposed system) ambayo inahitaji maoni ya wadau ili kuboresha Mfumo utakaopendekezwa ili kusaidia kuimarisha mawasiliano baina ya wadau wa usimamizi wa maafa.

“Mfumo huo utaboresha utaratibu wa kutoa tahadhari ya mapema kwa wadau na umma ili kuchukua hatua za haraka kwa ajili ya kuokoa maisha na mali,”alisisitiza Msangi.

Aidha, Sheria ya Usimamizi wa Maafa kifungu cha 4 imeelekeza kuweka mfumo wa teknolojia ya habari na mawasiliano utakaowaunganisha wadau wa masuala ya maafa ili kufuatilia mwenendo wa majanga na hali ya maafa kwa ajili ya kuchukua hatua za kuzuia na kukabiliana na maafa kwa wakati.

Idara ya Menejimenti ya Maafa itaendelea kuratibu na kusimamia masuala ya maafa nchini kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Usimamizi wa Maafa ya Mwaka 2004 na Sheria ya Usimamizi wa Maafa, Na. 6 ya mwaka 2022.

Kwa upande wake Mratibu Maafa UNICEF Bi.Judith ameeleza kuwa wataendelea kuboresha mashirikiano na wadau ili kuhakikisha wanajenga uwezo kwa wadau wa maafa katika ngazi zote kuanzia Taifa hadi vijiji.

“UNICEF tupo pamoja na tunaunga mkono jitihada zote zinazofanya na Seikali hivyo tutaendelea kuwajengea uwezo wadau wote na kuwafikia waathirika wa madhara yatokana ya maafa kwa lengo la kupunguza madhara hayo, na kuendelea kuboresha mifumo ya kupashanaji wa habari wakati wa maafa,”alisema Judith

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post