Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Elimu,Ubunifu na Utafiti kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Profesa Antony Mshandete akifungua kongamano la siku moja lililowakutanisha Wataalam kutoka Taasisi hiyo na Chuo Kikuu cha Dodoma pamoja na watunga sera wa Wizara mbalimbali katika kujadili Mradi wa Maabara ya Akili Bandia (Artificial Intelligence) leo Machi 29,2023 jijini Arusha.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Elimu, Utafiti na Ubunifu kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Profesa Antony Mshandete (Katika) akifuatilia majadiliano wakati wa kongamano la siku moja lililowakutanisha wataalam kutoka Taasisi hiyo na Chuo kikuu Dodoma pamoja na watunga sera wa wizara mbalimbali kujadili maendeleo ya mradi wa Maabara Bandia leo Machi 29,2023 jijini Arusha. Kushoto ni Mhadhili kutoka UDOM Dkt. Ally Nyamawe na kulia ni Mkurugenzi wa Utafiti na Huduma Elekezi za Jamii UDOM Profesa Ambrose Kessy.
Wataalam kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela na Chuo kikuu cha Dodoma pamoja na watunga sera kutoka wizara mbalimbali wakifuatilia na kujadiliana kwa pamoja kuhusu mchango wa Mradi wa Maabara Bandia katika kutatua changamoto mbalimbali katika jamii wakato wa Kongamano la siku moja lililofanyika leo Machi 29,2023 jijini Arusha.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma ,Utafiti na Ubunifu Profesa Antony Mshandete akiwa katika Picha ya pamoja ( katikati waliokaa) na washiriki wa kongamano la siku moja la mradi wa Maabara ya Akili Bandia kwa Maendeleo ya Afrika leo Machi 29,2023 jijini Arusha
Na Mwandishi Wetu-Arusha
Wataalamu kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wamekutana na watunga Sera kutoka wizara mbalimbali katika kongamano la siku moja kujadiliana jinsi gani mradi wa maabara ya Akili Bandia kwa Maendeleo ya Afrika(Artificial Intelligence) utakavyoweza kutatua changamoto zinazoikabili jamii katika magonjwa na mifugo.
Akifungua kongamano hilo leo Machi 29 , 2023 Jijini ArushaNaibu Makamu Mkuu wa Chuo Elimu, Utafiti na Ubunifu kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayamsi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Anthony Mshandete amesema lengo la kongamano hilo ni kukutanisha wataalam hao pamoja na watunga sera ili kubaini jinsi gani Kompyuta inavyoweza kufanya kazi katika tafiti, bunifu na kilimo ikiwemo kubaini aina za magonjwa kwa binadamu na mifugo.
Prof Mshandete ameeleza kuwa, mradi wa Akili Bandia ni mradi mkubwa wa kisayansi itakayotumika kwa ajili ya kubaini magonjwa mbalimbali ya wanyama na binadamu ili kuyadhibiti hivyo ni vyema watunga sera waujue, ili waweze kuuingiza katika miongozo mbalimbali itakayosaidia wizara mbalimbali kubaini magonjwa yanayoibuka kwa haraka kwa kutumia kompyuta.
"Teknolojia hii ni mpya ambayo hubaini kwa haraka magonjwa ya aina mbalimbali yanayoibuka kwa wanyama na binadamu pia itamsaidia mfugaji kubaini changamoto zinazowakabili na kudhibiti magonjwa kwa haraka zaidi" anasema Profesa Mshandete
Naye Mtafiti Mkuu wa Mradi huo wa Akili Bandia (AI4D Research Lab Project) Dkt. Ally Nyamawe amesema, mradi huo wa kisayansi unagharimu kiasi cha sh.Bilioni 1.8 utasaidia watafiti kubaini kwa haraka aina mbalimbali za magonjwa kwa binadamu na wanyama na namna ya kudhibiti.
Ameongeza kuwa, teknolojia hiyo ili iweze kushika kasi zaidi ni vyema watunga sera na watoa maamuzi kuelewa mradi huo katika tafiti, bunifu na mafunzo ili kuwezesha kubaini changamoto katia sekta ya kilimo, uchumi wa kidigitali, afya ikiwemo kubaini wabunifu katika kutatua matatizo tofauti katika jamii hususan kilimo, afya na mifugo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utafiti na Huduma Elekezi za Jamii, Profesa Ambrose Kessy kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma ameeleza kuwa mfumo huo hauchukui akili za biandamu bali ni msaidizi katika kubaini na kuleta matokeo ya haraka katika jambo lililoibuka hususan katika milipuko ya magonjwa kwa wanadamu na wanyama.
Mradi huo umefadhiliwa na Mashirika ya IDRC -Canada na Sida -Sweden kupitia mradi wa AI4D Afrika Program.
Social Plugin