WAZIRI MABULA AZINDUA KITABU CHA BUILDING THE JUST CITY IN TANZANIA


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akionesha kitabu cha Building the Just City in Tanzania baada ya kukizindua jijini Dodoma Tarehe 21 Machi 2023. Kulia ni Meya wa jiji la Dodoma Profesa Davis Mwamfupe na kushoto ni Dkt Tatu Limbumba kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizindua kitabu cha Building the Just City in Tanzania jijini Dodoma Tarehe 21 Machi 2023. Kulia ni Meya wa jiji la Dodoma Profesa Davis Mwamfupe na kushoto ni Dkt Tatu Limbumba kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Building the Just City in Tanzania.

Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Friedrich-Ebert-Stiftng (FES) Elisabeth Bollrich akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Building the Just City in Tanzania jijini Dodoma Tarehe 21 Machi 2023.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Friedrich-Ebert-Stiftng (FES) alipowasili kuzindua kitabu cha Building the Just City in Tanzania jijini Dodoma tarehe 21 Machi 2023.

Sehemu ya washiriki wa uzinduzi wa kitabu cha Building the Just City in Tanzania jijini Dodoma Tarehe 21 Machi 2023. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

***************************

Na Munir Shemweta, WANMM

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amezindua kitabu kinachojulikana kwa jina la Bulding the Just City in Tanzania: Essays on Urban Housing kilichoandaliwa na taasisi ya Friedrich-Ebert-Stiftng (FES).

Kitabu hicho ambacho ni mkusanyiko wa insha zenye maudhui yaliyobeba jumbe mbalimbali zinazotoa mchango katika kupanga na kuendeleza miji na mfumo wa utawala unavyoweza kuathiri upatikanaji wa nyumba za gharama nafuu kwa wote na masharti au utaratibu wa upatikanaji ardhi ambayo ndiyo msingi wa upataikanaji wa nyumba.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho jijini Dodoma tarehe 21 Machi 2023 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewataka wadau wa sekta ya uendelezaji milki kusaidiana na serikali kuogeza kasi ya ukuzaji miji iliyosalama na iliyopangwa vyema.

Ameongeza kwa kusema kuwa, wadau wa upangaji na upimaji wanakaribishwa ili kuongeza kasi ya upangaji na upimaji ardhi ili kuwezesha watanzania kupata ardhi iliyopangwa na kupimwa ili kuepusha ama kuondokana na ujenzi holela na hivyo kuwa na miji inayokuwa katika utaratibu uliopangwa.

"Nimegundua kuwa kuna mapendekezo ya kisera kwa serikali kuu, mamlaka za serikali za mitaana wadau wengine ambayo yote yanalenga kuchangia kuboresha upatikanaji wa nyumba za bei nafuu zinazotosheleza, zinazofaa na salama" alisema Dkt Mabula.

Kwa upande wake Mstahiki meya jiji la Dodoma Profesa Davis Mwamfupe alisema miji mingi uendelezaji wake unaenda tofauti na mipango kabambe kutokana na uwezo mdogo wa halmashauri katika kutekeleza mpango huo jambo alilolieleza kuwa linachangia ukuaji wa miji holela.

‘’Implementation ya master plan, kwa upande wangu naona halmashauri zina uwezo mdogo wa kusimamia, serikali kuu inatakiwa kuwa mdau mkubwa katika suala hili’’ alisema Profesa Mwamfupe.

Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi Friedrich-Ebert-Stiftng(FES) Elisabeth Bollrich alisema kitabu hicho chenye mkusanyiko wa insha mbalimbali kinaelezea na kutoa mchango mkubwa katika masuala ya kupanga na kuendeleza miji sambamba na wajibu wa serikali kuwezesha upatikanaji wa makazi ya bei nafuu na ya kutosha na kuondoa changamoto katika upatikanajj wa nyumba nchini.

Kitabu cha Building the Just City in Tanzania kimeandaliwa na kundi la wasomi wenye fani mbalimbali wanaojulikana kama Just City Platform (JCP) Tanzania kwa ufadhili wa Shirika la FES kikiangazia mijadala muhimu kuhusiana na changamoto zilizopo katika uendelezaji miji Tanzania.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم