***************
Na Mwandishi Wetu, Mtwara
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof.Joyce Ndalichako amewaasa wajasiriamali mkoani Mtwara kutumia Mwenge wa Uhuru kama chachu ya kukuza biashara na huduma.
Akifungua maonesho ya biashara, uwekezaji na fursa kwenye viwanja vya mashujaa park Mtwara Machi 30, 2023, Prof. Ndalichako, amesema kupitia Mwenge fursa mbalimbali ziibuliwe na kutengeneza ajira huku akiwapongeza walioona fursa na kuzitumia. Aidha, amelitaka Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) kuweka mkakati endelevu wa kuwasaidia wajasiriamali hao kupata masoko ya kudumu nchini na nje ya nchi.
“Wajasiriamali kumbukeni kuwa soko la Afrika Mashariki lipo wazi kwa nchi zote wanachama hivyo tuwe wabunifu ili kuweza kulitumia soko hilo na kuonesha ushindani wa bidhaa baina yetu na wenzetu,”amesema.
Social Plugin