NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KLABU ya yanga imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali kwnye michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kuichapa US Monastir kwa mabao 2-0, kwenye mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Yanga Sc ilianza kupata bao kipindi cha kwanza kupitia kwa Kennedy Musonda akipokea krosi kutoka kwa winga wao machachali Jesus Moloko na kuzamisha wavuni.
Kipindi cha pili Yanga ilirudi ikiwa inalisakama lango la mpinzani wake na kuweza kufanikiwa kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wao Fiston Mayele licha ya kukosa nafasi nyingi za mabao.
Social Plugin