Meneja wa Nyanda za Juu Kusini Dkt. Samweli Jasper akionesha shehena ya unga unaosagwa katika kiwanda chao na kuhifadhiwa vizuri.
Na Mwandishi wetu,IRINGA.
BODI ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) imetekeleza kwa vitendo juhudi za Rais Samia Suluhu Hassani katika kukuza sekta ya Kilimo nchini, kwa kuwahudumia wananchi na kuwapa ahueni kwa kuwauzuia bidhaa zao kwa bei nafuu na zenye ubora.
Aidha CPB imelenga kukuza Uchumi wa Nchi na Mwananchi mmoja moja kwa kuuza bidhaa zao nje ya nchi na ndani ya nchi lakini katika ubora unaozingatia Afya kwa maana ya kuhakikisha virutubisho vyote vilivyomo katika Nafaka vinakuepo katika bidhaa zao.
Meneja wa Nyanda za Juu Kusini wa CPB Dkt Jasper Samweli amesema hayo mkoani hapa wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu bodi hiyo inavyosimamia sekta ya kilimo na kueleza kuwa ipo kwa ajili ya Wananchi kwa kuwapa bidhaa iliyo na kuwauzia kwa bei nafuu kwani hilo ndio lengo la Serikali ya Rais Samia.
‘’CPB inamuunga mkono Rais Samia kwa vitendo kwa kutoa huduma iliyo bora kwa Wananchi kuhakikisha wanakula vyakula vilivyopimwa na kuchakatwa kwa usahihi bila kupoteza virutubisho vilivopo katika mazao’’, alisema Dkt. jasper amesema.
8
Aidha Meneja huyo amesema Rais Samia Suluhu ametoa zaidi ya Billioni 200 katika sekta ya Kilimo hivyo CPB haina budi kufanya kazi kwa uhakika na umakini ukilenga kuwasaidia wananchi katika kupata chakula bora.
Meneja huyo amesema kuwa CPB Nyanda za Juu Kusini wamekuwa wakihudumia katika Mikoa ya Mbeya, Ruvuma, Songwe, Njombe na Iringa yenyewe hivyo wananchi wa ukanda huo wamekuwa wakipata huduma ya kuuziwa bidhaa zao na kunufà ika kupitia sekta hiyo.
"Lengo la CPB ni kuinua Uchumi wa mtu mmoja mmoja lakini na wa Nchi pia, hivyo tunanunua mazao kutoka kwa wakulima wa ukanda huu na kuyachakata, kusindika na kusaga alafu tunawauzia bidhaa zetu kwa bei nafuu ukilinganisha bei za sehemu nyingine’’, amesema Meneja huyo.
Amesema katika kukuza Uchumi wa Nchi CPB imekuwa ikiuza bidhaa zake nje ya nchi kama vile Rwanda, Kenya na Malawi na kwamba bidhaa zao zipo katika kila ujazo kwani wanauza rejereja na jumla hivyo wamekuwa wakiuzia wafanyabiashara wakubwa,wakati na wadogo pamoja na wananchi wa kawaida.
‘’Tuna mtambo ambao una uwezo wa kuzalisha tani 50 hadi 55 za mahindi kwa siku ambao ukisagwa zinatoka tani 45 za unga,ni juhudi kubwa ambayo imetokana na Serikali, ili kuwafikia wananchi wote CPB inatarajia kuweka Mawakala wa bidhaa zao kila Mkoa ambao watakuwa wakisambaza bidhaa hizo,"anafafanua Meneja huyo.
Social Plugin