Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma Marco Chilya, akitoa taarifa ya vifo vya watu 13 na majeruhi wawili katika chumba cha kuhifadhia maiti.
Na Cresensia Kapinga ,JamhuriMedia, Songea
Wafanyabiashara 13 wamefariki na wengine wawili wamejeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutumbukia mto Njoka wakati wakitoka Ndongosi mnadani kuelekea kijiji cha Namatuhi wilayani Songea mkoani Ruvuma.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 10, 2023, kwenye eneo la chumba cha kuhifadhia maiti kilichopo Hospitali ya Serikali ya Mkoa Songea (HOMSO), Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Marco Chily,a amesema kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 3, usiku katika eneo la daraja la Mto Njoka Namatuhi katika barabara ya Ndongosi iendayo Namatuhi Songea vijijini.Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Mkoa wa Songea (HOMSO), Dkt Magafu Majur , akizungumza na waandishi wa habari kwenye chumba cha kuhifadhia maiti .
Amesema kuwa gari hilo lenye namba za usajili T 800 BXB, Mistubish Fusso, lililokuwa likiendeshwa na dereva Thobias Njovu, lilipofika kwenye eneo la daraja hilo na wakati linapanda mlima ghafla liliacha njia na kutumbukia mtoni .
Amewataja wafanyabiashara walifaofariki kwenye ajali hiyo kuwa ni Happy Msemwa, Jafari Ngalimus, Hidaya Salum,Biesha Yahaya ,Mustafa Ally, wengine wamefahamika kwa jina moja moja ambao ni Mwaisha, Hamad, Juma Said ,Boniface, Christofa Msuya.
Wengine ni Deograsia Mapunda, Simba na mama Faraja ambapo majeruhi ni Hamis Mbawala na Christofa Banda ambao wamelazwa katika kituo cha afya cha Mpitimbi.
Kamanda amesema kuwa maiti zimehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Serikali ya Mkoa wa Songea.
Aidha Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linaendelea kusisitiza wananchi kuacha kupanda magari ya mizigo wanapokuwa wanakwenda kwenye minada hivyo Polisi hawatosita kuchukua hatua kali dhidi ya yeyote atakayekiuka agizo hilo.Baadhi ya wananchi waliofika kutambua miili ya ndugu zao kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya serikali ya Mkoa wa Songea (HOMSO)
Chanzo - Jamhuri
Social Plugin