Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir amesema Sikukuu ya Eid el-Fitr itakuwa Jumamosi ya Aprili 22, 2023.
Sikukuu hiyo Kitaifa itafanyikia jijini Dar es Salaam ambapo Swala ya Eid itaswaliwa Msikiti wa Mfalme Mohamed VI Bakwata Makao Makuu, Kinondoni kuanzia saa 1:30 asubuhi na kufuatiwa na Baraza la Eid litakalofanyika ukumbi wa Mwalimu Nyerere kuanzia saa 8:30 mchana.
Katika Baraza hilo, inatarajiwa kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiongozwa na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Social Plugin