Mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi wilaya ya Lindi imemhukumu Said Mohamed (49) mkazi wa chikonji Lindi, kifungo cha miaka 30 jela sambamba na adhabu ya viboko 6 na kulipa fidia ya shilingi laki tano kwa kosa la kumbaka bibi wa miaka 62 katika kijiji cha Chikonji manispaaa ya Lindi.
Hukumu hiyo imetolewa na hakimu mkazi mfawidhi Maria Batulaine ambapo imetolewa kwa mujibu wa kifungu cha 130(1)(2)(a) na 131(1) cha kanuni ya Adhabu
Inaelezwa kwamba mtuhumiwa alimvizia na kumpiga mtama bibi huyo nyakati za saa 11 Alfajiri wakati ambao bibi huyo alikuwa akielekea shambani na kumbaka.
Upande wake mtuhumiwa ameiambia mahakama kuwa hajatenda jambo hilo hivyo sheria izingatie suala lake kwani amesingiziwa. Huku jopo la mashahidi wanne ambao ni mtaalamu wa Afya (Daktari), mwenyekiti wa kijiji, mgambo aliyeshiriki kumkamata mtuhumiwa na mtendwa mwenyewe, wamekiri kutokea kwa tukio hilo
Baada ya Hukumu hiyo ya kifungo cha miaka 30 jela, adhabu ya viboko 6 na kumpa fidia ya shilingi laki 5 mtendwa hakimu Maria Batulaine ametoa nafasi kwa mtuhumiwa kukata rufaa.
Social Plugin