Akiwa mjini,humo Lembeli alitarajiwa kuhudhuria sherehe maalum ya kutimiza miaka 89, muasisi wa taasisi ya Jane Goodall ambayo chimbuko lake ni Hifadhi ya Taifa ya Gombe,Kigoma ambako alifika mwaka 1960 kuanzia kufanya utafiti wa mnyama aina ya sokwe.
Utafiti huo wa Sokwe,umedumu Kwa zaidi ya miaka 60 na unaendeshwa na taasisi hiyo ya Jane Goodall ambao hivi Sasa unaendeshwa na watanzania.
Jane Goodall,raia wa Uingereza pia ni Balozi wa heshima wa Umoja wa Mataifa wa Amani.
Sherehe hiyo,ilihudhuriwa na wanasayansi na viongozi mashuhuri mbalimbali wa nchini Marekani.
Aidha Lembeli atahudhuria kikao cha Bodi ya Wakurungenzi ya Jane Goodall-Marekani ambako yeye ni mjumbe pekee toka Afrika.
Taasisi ya Jane Goodall ambayo Ina ofisi katika nchi zaidi 100 ulimwenguni inajihusisha hasa na utafiti na uhifadhi wa Sokwe barani Afrika na jamii ya wanyama aina ya nyani.
Nchini Tanzania,mbali ya utafiti katika Hifadhi ya Gombe,taasisi hiyo inaendesha miradi mbalimbali ya uhifadhi wa mazingira hasa misitu ya asili sambamba na miradi ya afya na maendeleo ya jamii ktk mikoa ya Kigoma na Katavi.
Lembeli,ambaye ni Mwenyekiti wa taasisi hiyo hapa nchini aliwahi pia kuwa Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Mazingira ambaye ripoti yake juu ya madudu yaliyojitokeza katika utekelezaji wa operesheni tokomeza ilipelekea mawaziri watatu kutumbuliwa na mmoja kujiuzulu.
Lembeli anatarajiwa kurudi nchini tarehe 13.4. 2023.
Social Plugin