Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MLINZI AUAWA KWA KUCHINJWA MSIKITINI MJINI KAHAMA



Na Mwandishi Wetu - Malunde 1 blog
Mlinzi Kampuni binafsi ya ulinzi Bakari Kasarani (46) ameuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana katika msikiti wa Shree Hindu Mandal Temple Mjini Kahama mkoani Shinyanga.

Inaelezwa kuwa mlinzi huyo aliyefanya kazi katika msikiti huo kwa miaka 10 ameuawa Machi 30,2023 usiku akiwa katika msikiti akiendeleana kazi yake ulinzi ambapo pia wahalifu waliharibu vitu vya thamani mbalimbali zilizopo ndani ya Msikiti huo ikiwemo sanamu ya kuabudia.

Akisimulia kuhusu tukio hilo, Msimamizi wa msikiti huo Niraj Kakad amesema mlinzi huyo alikutwa ameuawa nyuma ya msikiti na vitu ambavyo bado thamani yake haijajulikana vimevunjwa ikiwemo sanamu inayoabudiwa.


Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na usalama ya mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amelaani tukio hilo la kikatili na kuagiza watu waliofanya unyama huo watafutwe mara moja ili hatua za kisheria zichukuliwe.

Mndeme amesema serikali itagharamia uharibifu uliofanywa ndani ya msikiti huo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com