Maafisa kutoka Kitengo cha Upelelezi wa Jinai nchini Kenya bado wanaendelea kupiga kambi katika msitu wa Shakahola huko Malindi wakichunguza zaidi miili ya wafuasi wa Mchungaji Paul Mackenzie.
Maafisa hao wamekwishatoa miili ya watu 47 ambao wanadhaniwa kuwa wafuasi wa Pasta huyo.
Kwa upande wao, Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya limetangaza kuwa limeweka vituo vya kuwasaka watu na kuwapa ushauri katika Hospitali ya Wilaya ya Malindi kwa ajili ya kusaidia jamii ya Shakahola.
"Tumeweka vituo vya kuwasaka watu na kuwapa ushauri katika Hospitali ya Wilaya ya Malindi kwa ajili ya kusaidia jamii ya Shakahola. Hadi sasa watu 112 wameripotiwa kupotea katika kituo cha kuwasaka watu," ilisema taarifa ya Msalaba Mwekundu Kenya.
Jumapili, Aprili 23, 2023 walifukua miili mingine 18 iliyozikwa kwa kina kifupi na kuongeza idadi ya miili iliyokwishafukuliwa hadi 47.
Social Plugin