Video inasambaa mitandaoni ikionyesha tukio ambapo mwalimu wa kike na mwanafunzi wa kike walikuwa wakipigana darasani.
Tukio hilo linaripotiwa kutokea Jumatatu, Aprili 17, 2023 katika Shule ya Upili ya Rocky Mount, kaunti ya Nash, jimbo la North Carolina, Marekani.
Kulingana na ripoti, Xaviera Steel, ambaye alikuwa akifunza kama mwalimu mbadala katika shule hiyo, anasemekana kumpokonya mwanafunzi huyo simu alipokuwa akiitumia darasani.
Kisha mwanafunzi huyo aliyekuwa amekereka, alimkaripia Steel, akitaka amrejeshee simu yake, akisema kuwa sheria hazitumiki kwa kila mtu na kusisitiza kwamba ilikuwa simu yake.
"Kwa nini sheria hazitumiki kwa kila mtu mwingine. Hiyo ni simu yangu,” mwanafunzi huyo alisikika akisema. Mwalimu Steel alimjibu kuwa sheria hizo zinatumika kwa kila mtu, huku akimwonya mwanafunzi huyo kutomgusa.
Lakini mwanafunzi huyo alimrukia, hali ambayo ilichochea vita vikali kati ya wawili hao. Polisi wa Rocky Mount walithibitisha tukio hilo na kuongeza kuwa hakuna aliyejeruhiwa.
School teacher beats up student for slapping her https://t.co/ipdevL0wsa
— YabaLeftOnline (@yabaleftonline) April 18, 2023
Social Plugin