Aliyewahi kuwa Mbunge wa Butiama mkoani Mara, Nimrod Mkono amefariki dunia akiwa nchini Marekani alikokuwa akitibiwa tangu mwaka 2018 akisumbuliwa na ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).
Inaelezwa kuwa Mkono alikuwa anatibiwa nchini Marekani katika jimbo la Florida kwa takribani miaka mitano.
Mkono aliyezaliwa Agosti 18, 1948, Busegwe Mkoani Mara alikuwa mwanasheria na mwanasiasa maarufu.
Mwenyekiti mstaafu wa CCM Mkoa wa Mara, Samuel Kiboye maarufu Namba tatu amesema kuwa chama hicho kimepoteza kada mtiifu na mpenda maendeleo wa kweli.
Social Plugin