TAASISI MBILI ZA ELIMU ZAPATA MSAADA WA DOLA 20,000 KUTOKA SHIRIKA LA NVEP KWA UFADHILI WA BARRICK


Meneja wa Barrick Nchini Tanzania, Melkiory Ngido(kulia) akikabidhi hundi ya dola za Kimarekani milioni 10 kwa Mkurugenzi wa mipango kutoka taasisi ya TanSAF ,Alex Elifas (wa pili kutoka kulia aliyeambatana na wanafunzi waliopo kwenye programu za taasisi hiyo Bruno Basley Bruno (kushoto) na Isaya Charles.
Meneja wa Barrick Nchini Tanzania, Melkiory Ngido(kulia) akikabidhi hundi ya dola za Kimarekani milioni 10 kwa Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilosa, Wapa Mpwewe wa pili kulia aliongozana na viongozi wa shule hiyo.
Meneja wa Barrick Nchini Tanzania, Melkiory Ngido (katikati mwenye shati la bluu) akiongea katika hafla ya kukabidhi msaada wa dola za kimarekani 20,000 kwa taasisi mbili za hapa nchini kwa ajili ya kuboresha elimu.
Watendaji kutoka taasisi zilizopata msaada wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Barrick Nchini Tanzania, Melkiory Ngido na Wafanyakazi waandamizi wa Barrick nchini.
Wanafunzi waliohudhuria hafla hiyo ambao wako katika programu wa kutafutiwa masomo na taasisi ya TanSAF wakiwa pamoja na Afisa Mawasiliano wa Barrick, Abella Mutiganzi.

****
Shirika la ya Nos Vies en Partage (NVeP) kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick,wametoa msaada wa dola za kimarekani 20,000 kwa taasisi isiyo ya Serikali ya Tanzania Student Achievement Foundation (TanSAF) na shule ya sekondari ya Serikali ya Parakuyo iliyopo wilayani Kilosa mkoani Morogoro kwa ajili ya kusaidia kuboresha mazingira ya wanafunzi wanaosoma katika mazingira magumu.


Msaada huo umetokana na sehemu ya fedha zilizotolewa na taasisi ya Nos Vies en Partage (NVeP), iliyoanzishwa na inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow, kwa ajili ya kusaidia makundi maalum kama vile Wanawake,watoto na makundi mengine yenye uhitaji yasiofaidika na ukuaji wa kiuchumi barani Afrika.

Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Meneja wa Barrick Nchini Tanzania, Melkiory Ngido, alisema kila robo ya mwaka,taasisi imeweza kutoa misaada yenye tija na manufaa ya moja kwa moja kwenye jamii zenye uhitaji.

“Hadi sasa tumeweza kutoa msaada kwa zaidi ya mashirika 10 nchini Tanzania kupitia taasisi ya NVeP ,lakini huu ni mwanzo,leo tuko hapa kuleta mabadiliko katika taasisi mbili kwa kuzipatia msaada wa dola za Kimarekani 10,000 kila moja kwa ajili ya kuboresha elimu kwa watoto’’, alisema Ngido.

Akiongea baada ya kupokea hundi ya fedha za msaada huo, Mkurugenzi wa mipango kutoka taasisi ya TanSAF, Alex Elifas, alishukuru kwa msaada huo na kueleza kuwa utasaidia kuwatafutia wenye vipaji kutoka familia zisizo na uwezo wa kifedha kutafutiwa fursa ya kusoma katika baadhi ya vyuo vikuu bora duniani kote.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilosa, Wapa Mpwewe, ambaye alipokea hundi kwa niaba ya Shule ya sekondari ya Parakuyo, alishukuru kupatiwa msaada huo na alisema kuwa utasaidia katika ujenzi wa mabweni ya wanafunzi ,“kwa bahati mbaya shule hii ilipata uharibifu kwa majengo kutokana na mvua kubwa za mafuriko mwaka jana,fedha hizi zinatasaidia kujenga upya nakuendelea kutoa elimu bora kwa wanafunzi wetu”alisema Mpwewe.

Akiongea kwa niaba ya wanafunzi waliohudhuria hafla hiyo, Bruno Bruno mhitimu wa kidato cha sita katika shule ya sekondari ya kisimiri iliyopo mkoani Arusha,alisema kuwa yuko katika mchakato wa kwenda kusoma elimu ya chuo kikuu nchini Marekani na amesaidiwa kutafuta chuo na Shirika la TanSAF.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post