Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) ambayo inatoa huduma katika Manispaa ya Shinyanga na Miji ya Didia, Tinde na Iselamagazi halmashauri ya Shinyanga imewafuturisha Wateja na Wadau wa SHUWASA Shinyanga ikiwa ni mwendelezo wa utamaduni wa Mamlaka hiyo kuungana na Waumini wa Dini ya Kiislamu wanaoishiriki Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Hafla ya Futari imefanyika leo Jumatatu Aprili 17,2023, katika ofisi za SHUWASA na imekuhudhuriwa na wateja na wadau wa SHUWASA wakiwemo Watoto wanaolelewa katika Kituo cha Buhangija kilichopo Mjini Shinyanga ambapo SHUWASA pia imekabidhi zawadi kwa watoto hao.
Akizungumza wakati wa Iftar hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi ambaye alikuwa mgeni rasmi ameishukuru na kuipongeza SHUWASA kuandaa Futari hiyo huku akiwaomba viongozi wa dini na jamii kuungana kupiga vitendo vya ukatili katika jamii.
“Vitendo vya ukatili ukiwemo ubakaji na vimeongezeka katika jamii, ni jukumu la kila mmoja wetu kupiga vita ukatili lakini pia kuhakikisha tunawalea watoto wetu ili kulinda maadili yetu na kuepuka mmomonyoko wa maadili kwa matendo maovu yanatupa taswira mbaya. Naomba viongozi wa dini mtilie mkazo suala la maadili ili tulinde jamii”,amesema Mhe. Samizi.
Akikabidhi zawadi ya sabuni, mafuta ya kupikia, sukari na juisi zilizotolewa na SHUWASA kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Mjini Shinyanga, Mkuu huyo wa wilaya amesema ni jambo jema kwa kila mwananchi pale anapopata chochote kuwasaidia watu wanaoishi katika mazingira magumu na wenye uhitaji.
Mwenyekiti wa Bodi ya SHUWASA Bi. Mwamvua Jilumbi amesema SHUWASA imekuwa na utamaduni wa kuandaa Futari kwa ajili ya wateja na wadau kutokana na kwamba waumini wa dini ya kiislamu ni sehemu ya wadau muhimu wa SHUWASA.
Amewaomba wananchi na wadau wote wa maji kuendelea kushirikiana na SHUWASA katika kulinda miundombinu ya maji sambamba na kutoa taarifa mbalimbali ili kuboresha huduma ya maji.
Sheikh wa Wilaya ya Shinyanga Soud Kategire na viongozi wa dini ya kiislamu na wadau wakichukua Futari.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa SHUWASA, Reuben Mwandumbya amewashukuru wadau wote walioshiriki katika futari hiyo na kuahidi kuwa SHUWASA itaendelea kuboresha zaidi huduma zake.
Naye Katibu wa Kamati ya Amani Wilaya ya Shinyanga Sheikh Shaban Katundu ameishukuru SHUWASA kuandaa Futari hiyo na kwamba viongozi wa dini ya kiislamu wataendelea kushirikiana na SHUWASA.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) leo Jumatatu Aprili 17,2023. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)
Katibu wa Kamati ya Amani Wilaya ya Shinyanga Sheikh Shaban Katundu akizungumza wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)
Kaimu Mkurugenzi wa SHUWASA, Reuben Mwandumbya akizungumza wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)
Mwenyekiti wa Bodi ya SHUWASA Bi. Mwamvua Jilumbi akizungumza wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)
Mwenyekiti wa Bodi ya SHUWASA Bi. Mwamvua Jilumbi akizungumza wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)
Mfanyakazi wa SHUWASA Kimbira Mtebe akizungumza wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)
Viongozi wa dini ya Kiislamu wakiomba dua wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)
Viongozi wa dini ya Kiislamu wakiomba dua wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akichukua Futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)
Sheikh wa Wilaya ya Shinyanga Soud Kategire na viongozi wa dini ya kiislamu na wadau wakichukua Futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akichukua Futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)
Waumini wa dini ya kiislamu na wadau wakichukua Futari
Waumini wa dini ya kiislamu na wadau wakichukua Futari
Watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija na wadau wakichukua Futari
Watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija na wadau wakichukua Futari
Wadau wakichukua Futari
Wadau wakichukua Futari
Wadau wakichukua Futari
Watoto wakipata Futari
Wadau wakipata Futari
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akikabidhi zawadi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) kwa ajili ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Mjini Shinyanga

Zawadi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) kwa ajili ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Mjini Shinyanga
Wafanyakazi wa Benki ya NBC wakipiga picha ya kumbukumbu na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi
Wadau wakipiga picha ya kumbukumbu
Meneja wa Benki ya CRDB Luther Mneney akibadilishana mawasiliano na mkazi wa Shinyanga Bw. Issa Mkondo (kushoto).
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog