Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JAMAA AMPA TALAKA MKEWE KISA KUDHARAU NDUGU NA MARAFIKI..."HADI MAMA YANGU ANAMUITA MCHAWI"


Mwanaume mmoja raia wa Ghana ametahamaki baada ya kufunguka kuhusu ndoa yake iliyofeli na aliyekuwa mkewe.

Akizungumza katika mahojiano na SVTV Africa kwenye YouTube, Agyei Mensa ambaye anaishi nchini Sweden alisema sababu kubwa iliyomfanya aondoke kwenye ndoa yake ya awali ni kutokana na tabia mbaya ya mkewe.

Akitafakari kwa kina, mlofa huyo alisema sifa moja ambayo hakuipenda kwa mke wake ni jinsi alivyowadharau jamaa na marafiki zake. 

Alieleza kuwa mke wake wa zamani hakuona kosa kuwatusi ndugu zake, marafiki na hata mama yake.

Alitaja jinsi mke wake wa zamani alivyokuwa na kiburi hadi kumshutumu mamaake kuwa mchawi ingawa ndiye aliyemshauri amuoe. 

“Mamangu ndiye alinishauri nimuoe mke wangu wa zamani lakini cha kushangaza baada ya kufunga ndoa mtazamo wake ulibadilika, ilifikia hatua anaweza kuwatukana ndugu, binamu na marafiki zangu waliokuja kunitembelea wakati wowote nikiwa Ghana. Wakati fulani alimuita mamaangu mchawi hivyo niliamua jambo bora zaidi kwangu ni kuvunja ndoa."

Aliongeza "hata nilikuwa nikitayarisha hati zake ili ajiunge nami Sweden ili tuishi kama familia yenye furaha, lakini mtazamo wake uliharibu kila kitu." 

Agyei Mensah alisema pamoja na kwamba ana mtoto wa miaka mitatu na mke wake wa zamani, anakusudia kumruhusu akue nchini Ghana ili apate malezi bora.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com