Mwanaume mmoja katika kijiji cha Chivovoli, kaunti ya Vihiga nchini Kenya anakumbana na mshtuko na huzuni baada ya mkewe kumtupa na kuolewa na jirani yake kwa sababu ya ufukara mkubwa nyumbani kwao.
David Sorema, anayefanya kazi za sulubu ambaye mara nyingi hupatikana katika mashamba ya chai, alikuwa na familia nzuri ya mke, wana watatu wa kiume na binti mmoja kabla ya mawimbi kupiga nyumba yake.
"Mama yangu sasa ni jirani yetu, alitutelekeza na kuolewa tena katika boma lilio karibu. Tangu aende baba yangu aligeuka kuwa mlevi siku nzima. Hawezi kutupatia mahitaji yetu ya kimsingi, tunakosa maji, mavazi, chakula, makazi yanayofaa," alisema mtoto wa David, Nickson Vuyekha katika mahojiano na mwanablogu wa You Tube Phelix Makanda.
Katika mahojiano na TUKO.co.ke, Makanda alisema Sorema aligeuka mraibu wa pombe kwa sababu ya msongo wa mawazo uliosababishwa na kumuona mkewe kila siku akiwa na jirani yake.
Kuongeza chumvi kwenye jeraha, watoto wawili wa Sorema walimtoroka naye binti yake aliwenda kuishi na mama yake katika boma la jirani na kusalia tu na kitina mimba wake Nickson.
Nickson ameshindwa kuenda shule na sasa ameamua kuuza vyuma vikuukuu sokoni. Wakati alipokuwa akihojiwa, kijana huyo alikuwa amepata KSh 40 pekee.
Shangazi yake Nickson alisema Sorema ni mwanaume asiyehajibika.
Alifichua kwamba walijaribu kumshauri kuhusiana na hali yake lakini alijitetea akisema maisha yalikuwa magumu sana.
Kulingana na Makanda, mvulana huyo anahitaji msaada kwani yuko katika hatari ya kuwa mtoto wa mitaani. Unaweza kumsaidia Nickson kupitia nambari 0713481436 (Phelix Joel).
Via Tuko News
Social Plugin