Waumini waa dini ya Kiislamu Wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamefanya maandamano ya amani ya kupinga na kulaani ndoa za jinsia moja, ushoga na usagaji.
Maandamano hayo ya kupinga vitendo vya mmomonyoko unaosababisha vijana kujiingiza katika makundi hatarishi ikiwemo matumizi ya dawa za kulevya na mapenzi ya jinsia moja kinyume na mafundisho ya Mwenyezi Mungu yamefanyika leo Jumamosi Aprili 30,2023.
Akizungumza wakati wa maandaamano hayo, Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Alhaj Ismail Habib Makusanya ameiomba serikali kudhibiti uanzishwaji holela wa baa katika makazi ya watu hali inayochochea uwepo wa vitendo vya ukiukwaji wa maadili.
Vitendo vya momonyoko wa maadili unaosabisha vijana kujiiingiza katika makundi yasiyofaa kutokana mabadiliko ya utandawazi
Social Plugin