Baadhi ya wananchi waliofika msibani kwa Jeni
Shabiki wa Yanga aliyejulikana kwa jina la Jane, mkazi wa Kata ya Bwilingu wilayani Chalinze mkoa wa Pwani, amepoteza maisha wakati akiangalia mchezo wa jana wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga.
Imeelezwa kuwa alipatwa na presha na kuanguka ghafla.
Mechi ya jana Aprili 16, 2023, Simba waliondoka na ushindi wa magoli mawili kwa nunge dhidi ya Yanga.
SIMBA SC iliendelea kupunguza gape la Pointi dhidi ya Yanga SC na kuendelea na mbio za Ubingwa baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Simba SC walianza kwa kasi ya ajabu na mnamo dakika ya 2 Beki Kisiki Henock Inonga aliwanyanyua mashabiki wake akifunga bao safi kwa kichwa akimalizia Krosi ya Shomari Kapombe.
Baada ya kupata bao hilo Simba waliendelea kuishambulia Yanga na dakika ya 32 Kiungo mshambuliaji aliyekubalika kwa mashabiki Kibu Denis alipigilia msumari wa pili kwa shuti kali lililomshinda Diarra.
Kwa ushindi huo Simba wamefikisha Pointi 63 na kupunguza gape la Pointi na kubaki alama tano huku kila timu ikibakiwa na mechi nne Ligi imalizike.
Yanga wanabaki na Pointi zao 68 ili wawe mabingwa wa Ligi msimu huu wanahitaji kushinda mechi tatu ili wafikishe Pointi 76 ambazo Simba akishinda mechi zake zote atakomea pointi 75 .
Social Plugin