Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANNE WATUPWA JELA MIAKA 20 KWA KUKUTWA NA PEMBE ZA NDOVU


Watu wanne wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 kwenda jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kukutwa na vipande tisa vya pembe za ndovu, kinyume cha sheria ya wanyama pori ya mwaka 2005 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2016 wakiwa katika hatua za mauzo ya nyara hizo za serikali.

Hukumu hiyo imetolewa katika mahakama ya hakimu mkazi Mkoa wa Shinyanga na hakimu mkazi Yusuph Zahoro, baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili na kuwatia hatiani washitakiwa wote wanne waliokuwa wanakabiliwa na Kesi ya uhujumu uchumi namba 1 ya mwaka 2022.

Washitakiwa hao walikutwa na vipande 9 vya pembe za ndovu vyenye thamani ya milioni 69.21 ambapo washitakiwa walikamatwa wakiwa katika hatua za kuuza nyara hizo kata ya Solwa wilaya ya Shinyanga.

Waliohukumiwa kifungo cha miaka 20 jela ni Emanuel Shija Basu, Shija Kaswahili, Revocatus Mtara na Daud Ndizu ambao walitenda kosa hilo July 13 , 2022 baada ya kukutwa na nyara za serikali kinyume cha sheria.

Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com