Mganga mkuu wa mkoa wa Dar es salam Dkt Rashid Mfaume atakuwa mgeni Rasmi katika Bonanza la uchangiaji damu salama litakalo fanyika tarehe 6 Mei wazo mivumoni.
Hayo yamesemwa na muandaaji wa Bonanza hilo Anjela Seth ambaye pia ni mwandishi kutoka fullshangweblog alipokuwa akiongea na wanahabari leo katika ufunguzi wa Ligi ndogo ya hamasa itakayochezwa kwa wiki mbili eneo la wazo huku timu kumi zikishiriki.
Aidha Anjela amesema nia na madhumuni ya ligi hiyo kuchezeshwa ni kutoa elimu na hamasa kwa wananchi juu ya uchangiaji damu salama kwa hiyari.
Kwa upande wake Mchungaji Richard Hananja ambaye ni mlezi wa Bonanza la uchangiaji damu salama Amesema anamshukuru Anjela kwa kuhamasisha uchangiaji wa damu salama kwani ni jambo jema na yeye yupo tayari kuendelea kuhamasisha viongozi wa Dini waweze kuhamasisha waumini wao kushiriki zoezi la uchangiaji damu salama kwa hiyari siku husika.
Naye Fatuma R. Mjungu ambaye ni Afisa Uhamasishaji kutoka Mpango wa Taifa Damu salama kanda ya mashariki amewahamasisha wananchi wa kata ya wazo, Wilaya kinondoni na mkoa kwa ujumla kushiriki zoezi la uchangiaji damu salama kwa hiyari siku husika.
Social Plugin