Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WADAU WAIPONGEZA WIZARA YA ELIMU KUANDAA WIKI YA UBUNIFU 2023 JIJINI DODOMA




Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akizungumza wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara hiyo yaliyomalizaka leo Aprili 28,2023 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Carolyne Nombo,akielezea malengo ya wiki ya ubunifu wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara hiyo yaliyomalizaka leo Aprili 28,2023 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof James Mdoe,akizungumza wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara hiyo yaliyomalizaka leo Aprili 28,2023 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.


Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, Elimu, Utamaduni na Michezo, Husna Sekiboko, ameipongeza Wizara ya Elimu kwa kuendeleza ubunifu na ugunduzi wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia yaliyomalizaka leo Aprili 28,2023 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.



Baadhi ya Wadau wakitoa salamu wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia yaliyomalizaka leo Aprili 28,2023 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.


Sehemu ya wageni wakifatilia hotuba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda (hayupo pichani),wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara hiyo yaliyomalizaka leo Aprili 28,2023 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akiwakabidhi Vyeti baadhi ya washindi wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara hiyo yaliyomalizaka leo Aprili 28,2023 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.



Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunga Kilele cha Maadhimisho ya Maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara hiyo yaliyomalizaka leo Aprili 28,2023 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akipata maelezo katika mabanda mara baada ya kufunga Kilele cha Maadhimisho ya Maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara hiyo yaliyomalizaka leo Aprili 28,2023 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,imesema masuala ya sayansi, teknolojia na ubunifu yanachochea kwa kasi maendeleo ya uchumi nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda katika Kilele cha Maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara hiyo yaliyomalizaka leo Aprili 28,2023 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Prof.Mkenda amesema sayansi, teknolojia na ubunifu una mchango mkubwa wa kuchagiza maendeleo ya kiuchumi na kwamba nchi mbalimbali zimefanikiwa kutokana na kuwekeza kwenye eneo hilo.

“Ibara ya 102 ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi inaahidi kuwa serikali itahakikisha inaendeleza sayansi, teknolojia na ubunifu, tunachokifanya hapa leo ni kuendeleza yale ambayo chama chenye serikali kilitoa ahadi wakati wa kuomba kura kwa wananchi, baada ya kufanya maonesho haya ya MAKISATU tunaona tunapata bidhaa zilizoibuliwa, zimebiasharishwa na ni jukumu letu kuzitangaza,”amesema Prof.Mkenda

Aidha Prof.Mkenda ameeleza kuwa Ilani ya CCM ilipoahidi kwa wananchi kuendeleza sayansi, teknolojia na ubunifu ni jambo kubwa sana na litakalowezesha nchi kusimama na mataifa mengine duniani bega kwa bega.

“Niwashukuru wadau mbalimbali ambao wameungana nasi kufanikisha maonesho haya napenda kutoa shukrani za pekee kwa UNDP na wadau wengine kwa kutushika mkono kupitia program ya FUNGUO, napenda kutaja benki ya NMB, CRDB, UNESCO, WFP,LM International TANZTECH hawa wataanza kuzalisha vishikwambi nchini na wataungana na sisi kupitia vyuo mbalimbali ili kusaidia wanafunzi wetu ili kuingia kwenye mafunzo maalum ya masuala ya kielektroniki na uhandisi,”amesema.

Hata hivyo Waziri Mkenda amewasisitiza vijana kusoma sayansi ili kuwa kupata wataalamu wa kutosha kwenye fani za sayansi na uhandisi.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, Elimu, Utamaduni na Michezo, Husna Sekiboko ameipongeza Wizara ya Elimu kwa kuendeleza ubunifu na ugunduzi hali itakayochagiza kufikia Tanzania ya Viwanda.

Awali Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Prof.Carolyne Nombo, amesema maadhimisho hayo ni sehemu ya mkakati wa serikali ya awamu ya sita katika kuongeza hamasa ya matumizi ya sayansi na teknolojia na ubunifu kama nyenzo muhimu ya kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Amesema tangu kuanzishwa kwa Mashindano ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) Mwaka 2019 wabunifu na wavumbuzi wachanga wapatao 2,636 waliibuliwa na kutambuliwa na Wizara.

“Wabunifu wengine 283 wanaendelezwa na serikali kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ili ubunifu wao ufikie hatua ya kuwa bidhaa na kuingia sokoni ili kuongeza fursa ya ajira na vipato kwa vijana wetu, wabunifu wachanga wanaendelezwa kwenye vituo atamizi na kumbi za ubunifu ambazo hadi sasa bunifu na teknolojia 53 zimefanikiwa kufikia hatua ya kuwa bidhaa na hivyo kutumika kutatua changamoto mbalimbali katika sekta ya kilimo, maji , madini, afya, elimu,”amesema.

Aidha ameeleza changamoto wanazokutana nazo wabunifu wachanga ni kukosa mahali pa kuendeleza bunifu zao na kwa kutambua hilo serikali kupitia taasisi ya COSTECH imeanzisha kumbi za ubunifu (Buni Innovation Hub) na atamizi za DTB kwa lengo la kuendeleza vijana wenye mawazo ya ubunifu mbalimbali.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com