Akizungumza leo Jumatatu Aprili 24, 2023 wakati wa shughuli hiyo, Inspekta Jenerali wa Polisi, Japhet Koome amesema baada ya kufika eneo la tukio na kushuhudia miili mingine 26 ikifukuliwa hivyo kufikia 65 waliokufa. Amesema watu 29 waliokolewa na kupelekwa hospitalini.
Jeshi hilo limeingia wasiwasi huenda baadhi hawakufa kwa njaa kabla ya kuzikwa kwenye eneo hilo.
Vyombo vya habari nchini Kenya vimeripoti mchungaji huyo alikamatwa siku 10 zilizopita na Jeshi la Polisi katika Kaunti ya Malindi nchini humo baada ya kudaiwa kuwashawishi waumini wake wafunge hadi kufa ili waingia mbinguni na kuurithi ufalme wa Mungu.
Social Plugin