Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Benson Ndiege akiwa amekaa katikati ya Timu ya Watumishi wa Tume ‘TCDC Ushirika Sport’ mara baada ya kikao na Timu hiyo ikiwa katika Mashindano ya Kombe la Mei Mosi 2023 Mkoani Morogoro
Picha mbalimbali za Watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) wakishiriki michezo mbalimbali Mashindano ya Kombe la Mei Mosi 2023 Mkoani Morogoro
Na.Mwandishi Wetu-MOROGORO
Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) Dkt. Benson Ndiege ametoa wito kwa Watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kutumia fursa za Michezo zinazojitokeza kujifunza mbinu mbalimbali na kuendeleza Michezo.
Ametoa wito huo alipotembelea kambi ya Michezo ya Watumishi wa Tume ya Timu ya ‘TCDC Ushirika Sports’ wakati wakiendelea kushiriki Michezo ya Kombe la Mei Mosi Mkoani Morogoro Aprili 21,2023
Mrajis amewataka Watumishi wa Tume kuzingatia masuala ya michezo kwa kushiriki na kubuni programu za Michezo zitakazo ongeza wigo wa ushiriki wa Watumishi pamoja na kuongeza ubora na ushindani wa Timu ya Tume, ili kuendeleza Michezo kwa afya na ufanisi kazini.
Mwenyekiti wa Timu ya Tume ‘TCDC Ushirika Sport’ Mrajis Msaidizi Ibrahim Kadudu akiongea kwa niaba ya wanamichezo hao ameshukuru Uongozi wa Tume kwa kuendelea kujitoa katika kuhakikisha Watumishi wanashiriki fursa mbalimbali za michezo zinazoongeza tija katika afya na maendeleo ya Watumishi.
‘TCDC Ushirika Sport’ imeshiriki Michezo ya Kombe la Mei Mosi 2023 katika michezo mbalimbali ikiwemo Mpira wa Miguu, Mpira wa Wavu, kuvuta Kamba na itaendelea na mingine iliyosalia kuelekea Siku ya Kilele cha Sherehe za Wafanyakazi Mei Mosi.
Social Plugin